Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwan M.Kikwete akiwasiri katika Kijiji cha Mindu Tulieni kwa nia ya kuwaomba Wananchi wa Kijiji hicho Kura ili awe Mbunge wao wa Jimbo la Chalinze.Ridhiwani alitembelea Vijiji vinne (4) vya Kata ya Lugoba.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani M.Kikwete akiweka saini yake katika kitabu cha wageni alipotembelea Kijiji cha Mindu Tulieni kilichopo kata ya Lugoba katika Jimbo la Chalinze
Katibu wa Itikadi na Uwenezi CCM Taifa Mh.Nape Nauye akiweka saini yake katika kitabu cha wageni pindi walipowasili katika Kijiji cha Mindu Tulieni katika Kata ya Lugoba.Wanakwaya wa Kijiji cha Mindu Tulieni Wakitumbuiza Mbele ya Mgeni Rasmi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete Hayupo pichani.
Wanakwaya wa jamii ya Kimasai wa Kijiji cha Mindu Tulieni Kata ya Lugoba wakitoa Burudani waliyoiandaa mbele ya Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete pamoja na Katibu wa Itikadi na Uwenezi CCM Taifa Mh.Nape Nauye hawapo Pichani.Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete akicheza Ngoma ya Kimasai na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mindu Tulieni Letema Sungwira pamoja na Wamasai wa Kijiji hicho.
Mgombea wa Ubunge kwa Tiketi ya CCM Jimbo la Chalinze Ridhiwani M.Kikwete akicheza Ngoma ya Kimasai pamoja na Wanawake wa Kimasai huko katika Kijiji cha Mindu Tulieni.Msanii wa kizazi kipya Samu wa Ukweli akitumbuiza katika Mkutano huo wa Mgombea Ubunge katika Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete uliofanyika katika Vijiji vitatu vya kata ya Lugoba Jimboni humo juzi.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi Katika Kata ya Lugoba akiimba na wenzake mbele ya Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete aliyeongozana na Katibu wa Itikadi na Uwenezi Mh.Nape Nauye hawapo pichani.
Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani M.Kikwete akiveshwa shingoni Cheni ya Heshima toka kwa Jamii ya Kimasai waliyomtunuku katika Kijiji cha Mindu Tulieni Kata ya Lugoba.
Diwani wa Kata ya Lugoba Mh.Rehema Mwene akimweleza Mgombea Ubunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani M.Kikwete Changamoto ambazo zinawakabiri Wanakijiji wa kata yake ya Lugoba ambazo zinaitajika kutatuliwa pindi akichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo.
Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Ridhiwani M.Kikwete akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Mindu Tulieni kata ya Lugoba jinsi atakavyotekeleza ahadi zake kwao pindi atakapochaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo lao la Chalinze.
Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani M.Kikwete akiwa na Katibu wa Itikadi na Uwenezi CCM Taifa Mh.Nape Nauye wakimuaga Mzee wa Kijiji cha Mindu Tulieni Mzee Sitoko Kakole aliyeketi katika Mkutano uliomalizika huko Kjijini.
Ridhiwani Mrisho Kikwete akiwaaga kwa kuwapungia Mkono Wananchi wa Kijiji cha Mindu Tulieni Kata ya Lugoba katika Jimbo la Chalinze.
Katika kuhakikisha anatekeleza ilani ya Uchaguzi Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Ridhiwani Mrisho Kikwete alifanya Kampeni katika Kijiji cha Mindu Tulieni kilichopo katika Kata ya Lugoba na Kupokelewa kwa Shangwe na Wananchi wa Kijiji hicho na kumtunuku Cheni ya Shanga Shingoni yenye maana ya heshima toka Jamii ya Kimasai inayoishi Huko.
Wakionyesha wanafuraha baada ya kutembelewa na Mgombea wao wanayempenda toka Chama cha Mapinduzi CCM Ridhiwani M.Kikwete Jamii hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa tawi la Mindu Tulieni Ndugu Pato Machana walimvisha nishani hiyo ya kuonyesha kuwa Wanampenda sana Ridhiwani Kikwete na Wanapenda awe Mbunge wao kutokana anayajua Vilivyo matatizo yao na anayeweza kuyatatua kwa kuwasaidia.
Akiongea kwa Furaha iliyopitiliza Diwani wa Kata Lugoba Rehema Mwene aliwaambia Wananchi wa Kijiji hicho kuwa Wasifanye Makosa siku ya Tarehe 6 Mwezi wa Nne wampigie Kura Ridhiwani Kikwete ili awe Mbunge wao ili ashirikiane nae kwa Kuwaletea Maendeleo kwa Kasi zaidi.
Mh.Diwani pia alimweleza Mgombea Changamoto zinazowakabiri wananchi wake na akamsihi pindi atakapopata nafasi ya kuwa Mbunge wao atashirikiana nae wazitatue ili kuwaletea Maendeleo kwa kasi zaidi ili Wananchi wanufaike zaidi.
Zifuatazo ni Changamoto zinazowakabiri wanakijiji wa kata ya Lugoba ambazo Mgombea Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete aliwaahidi Wananchi hao kuwa atazitekeleza kwa Uwadilifu Mkubwa kama Wananchi watampendekeza awe Mbunge wao.
1/HUDUMA ZA KIJAMII;
Mgombea alisema kuwa katika kuboresha Huduma za kijamii kama Elimu,Afya,na Malazi atahakikisha kuwa Huduma zote zinakuwa vizuri kwa kushirikiana na Serikali za Vijiji hivyo pamoja na Diwani wa kata hiyo.Atakuwa anashiriki katika Vikao vya Kijiji kila baada ya Mda ili kuweza kujua Maesabu yanayopatikana kupitia kodi za Wanakijiji ili kutunisha Mfuko wa Maendeleo.
2/MAJI:
Atawawezesha Wanachi kupata Maji safi ili kuepukana na Magonjwa yanayotokana na Maji yasiyo salama kwa kuweka Mashine zitakazokuwa zikipeleka Maji katika Visima Mbalimbali katika kila sehemu ya kijiji.
3/BARABARA:
Katika kuhakikisha Vijiji vinapata Maendeleo kwa kasi zaidi Mgombea Ridhiwani alisema kuwa Chanzo kwa Vijiji kupata Maendeleo ni Miundombinu ya Vijiji kuwa mizuri moja wapo ni Barabara kuwa nzuri zinazoweza kupitika bula buguza zozote zile na kusababisha Vijiji kupata Wawekezaji harak zaaidi.
4/MIGOGORO:
Kufuatana na Kijiji cha Mindu Tulieni kuwa na Wawekezaji wa Madini ya Kokoto na ambao walipoingia kuwekeza waliwaambia Wananchi ahadi kemkem ambazo hawajazitekeleza na kufikia sasa Wanawanyanganya Wananchi Ardhi kwa nguvu na Kujimilikisha wao wenyewe Mgombea aliwaambia Wananchi kuwa atahakikisha kuwa suala la Migogoro ya Ardhi analimaliza haraka liwezekanavyo ili Wananchi wanufaike kutokana ni Watanzania alafu wanahaki ya kumiliki Ardhi kwa mujibu wa Sheria.
CCM Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!
Imetayalishwa na Evance Willfredy
0 comments:
Chapisha Maoni