RIDHIWANI ATEMBELEA FAMILIA ILIYOFIWA NA WATOTO WAWILI KWA AJARI YA MAJI

 Hili ni shamba la Baba wa watoto wawili waliofariki katika Kisima cha Maji ambapo hili shamba ndipo walipozikiwa hao watoto.
 Baadhi ya Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM Walioongozana na Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete walipowasili kuuhani Msiba wa watoto wawili waliofariki kwa ajari ya maji huko Kiwangwa katika Jimbo la Chalinze.
Diwani wa Kata ya Kiwangwa katikati akiwa pamoja na M/Kiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Mh.Mzee Kazidi katika Msiba wa watoto wawili huko Kiwangwa. 
M/kiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Mh.Mzee Kazidi akitoa Salam za Rambi rambi kwa Familia iliyoondokewa na watoto wawili kwa ajari ya Maji huko Kiwangwa. 
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete akitoa pole kwa Baba na Mama wa watoto wawili Mariamu na Agnesi waliopoteza Maisha kwa ajeri y Maji huko Kiwangwa.
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete akiwafariji wanafamilia Baba na Mama William na Esther walioondokewa na watoto wao Huko katika kijiji cha Kiwangwa kata ya Kiwangwa.
Haya ni Makaburi ya Watoto wawili wa Familia Moja Waliofariki kwa Ajari ya Maji huko Kiwangwa

Katika kuhakikisha anapata nafasi ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete juzi alikuwa katika kampeni zake huko Kijiji cha Kiwangwa kata ya Kiwangwa  aliitembelea Familia ya ndugu William na Mkewe  bi Esther  iliopata Msiba wa kuondokewa na watoto wao wawili ambao walizama katika kisima walipokwenda kuchota maji katika kisima hicho.

Katika kufuatilia chanzo ni nini mpaka Watoto hawa walizama katika kisima hichi Wazazi Wanasema kama ifuatavyo:
               Mtoto mdogo Agness mwenye Umri wa Miaka mitatu (3) alienda kuchota Maji katika kisima kilichopo jirani na Nyumbani kwao huku akiongozana na Dada yake Mariam ndipo Mtoto huyu akadumbukia katika kisima hicho.

Dada yake Mariam alipomuona Mdogo wake kadumbukia katika Kisima hicho ndipo alipoamua aingie nae akamuokoe mdogo wake ndipo nae akazama katika Kisima hicho kilichokuwa na kina kilefu kidogo.

Baada ya kupita masaa kazaa Wazazi wakaamua kuwatafuta watoto wao bila mafanikio mpaka zikapita siku 2 ambapo wakazikuta Maiti hizo mbili katika Kisima Hicho ambazo zilianza kuharibika.

Baada ya hapo wakaitwa Majirani na ndugu wa Familia ili wazitoe Maiti hizo na shughuri za Mazishi zianze.akiongea kwa masikitiko makubwa Baba wa Watoto hao Bwana William anasema kuwa ni gafra sana na amepata mshtuko ambao unamfanya hasiamini kama Watoto wake wameondoka Duniani na Kufikilia kama kifo hicho si cha kupangwa na Mwenyezi mungu.

                   Mungu atoa na Mungu ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe,Amin.................................!!

                                       Imeandikwana na Evance Willfredy

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List