RIDHIWANI,KINANA WATIKISA KATA YA UBENA



Wananchi wa Kijiji cha Ubena wakicheza muziki uliokuwa ukitumbuizwa na Msanii wa Kizazi kipya Samu wa Ukweli wakijiandaa kumpokea Mgombea kiti cha Ubunge jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Ridhiwani M.Kikwete aliyeongozana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa mh.Abdurahamani Kinana. 

Wananchi wa Kijiji cha Ubena wakiwa wamejipanga kumpokea Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete aliyeongozana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Mh.Abdullahaman Kinana
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Mh.Abdullahaman Kinana kulia akiwa na Mgombea Ubunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete walipowasili katika kijiji cha Ubena kwa nia ya kuwaomba ridhaa kwa wananchi wa Kijiji hicho ili awe Mbunge wao.
Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Jimbo la Chalinze Ridhiwan M.Kikwete akiwahutubia Wananchi wa Kata ya Ubena.Katibu Mkuu wa CCM Taifa Mh.kinana alikuwepo kuhakikisha anamnadi Mgombea huyu anakuwa Mbunge wao.



Katibu wa CCM Taifa Mh.Abdullahaman Kinana akiwa ameongozana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani kikwete wakiwa wanawasili katika Kijiji cha Ubena kilichopo kata ya Ubena.


Msanii wa muziki Dokii akitumbuiza katika mkutano huo kwa ajili ya kumnadi Mgombea Ubunge wa jimbo la Chalinze kwa Tiketi ya CCM Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani Kikwete alipo wasiri katika kijiji hicho cha Ubena.
 
Msanii wa Muziki Afsa kazinja akiwatumbuiza Wananchi wa Kijiji cha Ubena katika kuhakikisha Mgombe Ridhiwani anapata Ubunge wa Jimbo la Chalinze.
Kikundi cha Ngoma za Asili cha Kijiji cha Ubena kilichopo katika Kata ya Ubena kikitumbuiza mbele ya Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani M.Kikwete akiwa na Katibu wa CCM Taifa Mh.Abdallahamani Kinana hawapo pichani.

Katibu wa CCM Taifa akimwelekeza jambo Katibu wa CCM wa Wilaya ya Bagamoyo katika Mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Ubena Kata ya Uena.

Ilikuwa siku ya Furaha sana kwa Wananchi wa Kijiji Cha  Ubena walipotembelewa na Katibu mkuu wa CCM Mh.Abdullahaman Kinana aliyeongozana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani Kikwete kwa nia ya kumnadi Mgombea Ubunge huyo.

Mkutano ulikuwa mzuri uliotawaliwa na Burudani za Ngoma toka katika Vikundi mbalimbali vya Kijijini hapo na Wasanii wa Muziki wa kizazi kipya wakiwamo Dokii,Afsa Kazinja,na Samu wa Ukweli waliotumbuiza kwa uhodari mkubwa na kuufanya Mkutano ufane.

Zifuatazo ni Changamoto za Kijijini hapo ambazo Mgombea Ubunge huyo aliziahidi kuzitatua pindi atakapokuwa Mbunge wao.

A/MAJI;
              Akiongea kwa Furaha ambayo aliipata baada ya kuwaona Wananchi wa Kijiji cha Ubena wakimshangilia kwa nyimbo na kumwambia kuwa asipate tabu kwa wao amepata Kura zote na watapenda awe Mbunge wao.Ridhiwani aliwaambia Wananchi hawa kuwa atashirikiana na Serikali ya Kijiji hiki pamoja na Diwani wake kuhakikisha anawaletea Maji safi kwa kuchimba Visima na kuweka Mabomba ambayo yatasafirisha Maji hayo safi.

B/ELIMU:
                 Mgombea Ubunge huyu Mwenye Umri wa Miaka 35 Ridhiwani M.Kikwete alisema kuwa analifahamu kwa kina tatizo la Elimu hususani maswala ya Shule kutokuwa na Madarasa ya kutosha,Waalimu kuwa wachache,Shule kutokuwa na vyoo na Maabara,Nyumba za Waalimu kuwa wachache na kutokuwepo na Shule za Waalimu.

                  Mjumbe huyu wa Halmashauri kuu CCM Taifa aliwahakikishia Wananchi wa Kata hii kuwa atafanya kila liwezekanaro Kutatua Changamoto hizi kwa kuziweka Shule zote za Jimboni kwake katika mazingiza yaliyo Bora ya kuwafanya Wanafunzi wanasoma katika Maingira mazuri.Ridhiwani Kikwete alisema kuwa Atajenga Shule na kuongeza Madarasa na kujenga Vyoo pamoja na kuwaajiri Waalimu wengi na kutengeneza Maabara za kisasa katika kutimiza Ilani ya CCM Inayosema Watanzania Laazima wapate Elimu.

C/AFYA:
               Kutokana na Wanawake kupata matatizo ya Kujifungua  na Kufariki wakiwa wanawaishwa kwenda kwenye Zahanati zilizokuwa mbali na Vijiji vyao,Ridhiwani aliwaambia Wananchi hawa kuwa atafanya kila liwezekanalo kuhakikisha anajenga Zahanati zilizo Bora na kuweka wauguzi wa kutosha ili kuondoa tatizo hili.

D/BARABARA;
                           Akimthibitishia Katibu Mkuu wa CCM Mh.Kinana,Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete alimwambia kuwa atahakikisha anatengeneza Barabara zilizo na Kiwango ili Wananchi wake wasipate tabu kwa kutoka Vijijini humo kwenda Sehemu nyingine.Pia alisema kuwa atajenga ili akaribishe Wawekezaji waweze kuingia katika Jimbo lake ili Wawekeze na Jimbo lake kupata Maendeleo na Vijana wake kupata Ajira.

E/MICHEZO:
                       Mjumbe huyu wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete aliwaambia Wananchi wa Kata ya Ubena kuwa ataanzisha Mashindano ya Michezo hasa kwa Vijana kama Mpira wa Miguu kwa Ajiri ya kumuenzi Mbunge aliyefariki Hayati Saidi Bwanamdogo na kuwapa pia kipaumbele wanawake kwa kuwaanzishi mchezo wa Mpira wa Pete.

                            CCM Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!
                                           Imetayarishwa na Evance Willfredy
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List