Jeska Daudi Ulumilwa Mwenyekiti wa UWT Kata ya Ubena akiwa na Miraji Mtaturu akiwaeleza Waandishi wa Habari jinsi Mjeruhiwa alivyo jeruhiwa na makada wa CUF katika Ofisi ya CCM Kijiji cha Tukamisasa kilichopo Kata ya Ubena Jimbo la Chalinze.
Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mh.miraji Mtaturu ambaye ndie anafuatilia kesi ya mjeruhiwa.Mgombea wa CUF ndiye anahusika kwa kumjeruhi mama Jeska Ulimilwa.
Mheshimiwa Katibu wa Itikadi na Uwenezi CCM Taifa Nape Nauye akieleza jinsi tukio hili lilivyomgusa na wanachama wa CCM kwa ujumla na kusema atahakikisha kuwa atalifanyia kazi kisheria zaidi.
Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani Mh mama Sauda Mpambalioto akiwaeleza Waandish wa habari toka vyombo mbalimbali jinsi alivyoguswa na jambo hili na kusema CUF wanatakiwa wachukuliwe hatua haraka ipasavyo hususani kiongozi aliyehusika kwa sababu kiongozi hatakiwi kuwa hivyo.
Mjeruhiwa Mwenyekiti wa UWT Kata ya ubena mama Jeska Ulimilwa akitoa maelezo kwa Waandishi wahabari jinsi ilivyotokea na Maumivu anayojisikia.
Mheshimiwa Katibu wa Itikadi na Uwenezi CCM Taifa akieleza jinsi alivyogusa na kitendo hichi kibaya kilichotendwa na Mgombea wa CUF akishilikiana na Wanachama wake katika Ofisi za CCM Kijiji.
Juzi Mnamo wa Tarehe 24/03/2014 kulitokea na ukatili wa ajabu ambao ulifanywa na Kiongozi Mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya Chama cha CUF Jimbo la Chalinze akishilikiana na Wanachama wake ambao kwenye mida ya saa nne hasubui walivamia Ofisi moja ya CCM iliyopo katika kijiji cha Tukamisasa Kata ya Ubena na kumjeruhi Mwenyekiti wa UWT Kata ya Ubena kwa kumnyonga mkono na kumvunja.
Akieleza kwa masikitiko zaidi jinsi alivyoguswa na suala hili,Katibu CCM Wilaya ya Mufindi Mh.Miraji Mtaturu kuwa kitendo walichofanya Wanachama wa CUF Wakiongozwa na Mgombea wa Ubunge Jimbo hili la Chalinze kwa tiketi ya CUF Ndugu Fabiani Sikauki kuwa ni kibaya na si uungwana kibinadamu na ni ukatili ambao unatakiwa kukemewa vikali na wahusika wachukuliwe hatua kali kwani wanafahamika na atalishangaa Jeshi la Polisi kama halito watia hatiani.
Naye Katibu wa Itikadi na Uwenezi CCM Taifa Mh.Nape Nauye alieleza jinsi hisia zake zilivyomgusa na kukemea vikari vitendo vya kinyama vinavyoendeshwa na Vyama vya Upinzani kwa kuwatendea vitendo vya ukatili Wanachama wa CCM kama kuwapiga,kuwavuanguo,kuwaibia vitu,na kuwadharirisha.
Wanachama hawa wa CUF walivamia Ofisi hiyo ya CCM kwa kujitambulisha kama ni Maofisa Usalama wa Taifa na kuwakuta na kitabu cha wapigia kura ndipo wakaanza kuwashambulia na mmoja wa mama aliyekuwa na Mjeruhiwa alifanikiwa kutoloka na kuwaacha wakimshambulia mama Jeska ambaye walifanikiwa kumvunja mkono na aliyemtambua ni Mgombea wa Ubunge kupitia Chama cha Wananchi (CUF) ndugu Fabiani Sikauki.
Naye shahidi aliyekuwepo katika tukio hilo Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Kata na Mwenyekiti wa Kijiji cha Tukamisasa Ndugu Shabani Seif alisema kuwa wanachama hao wakiongozwa na Mgombea wao wa Ubunge kwa tiketi ya CUF Ndugu Fabiani Sikauki walivamia katika mida ya saa 4 hasubui huku wakijitambulusha kuwa ni Maafisa usalama walipokalibishwa wakaanza kuleta fujo kwa kuwapiga na wengine kufanikiwa kukimbia.
"Nitalifuatilia kwa undani zaidi kuhakikisha Mgombea Ubunge wa CUF Jimbo la chalinze Ndugu Fabiani Sikauki anachukuliwa hatua,Nitawashangaa Askari Polisi kama watashindwa kumkamata mshtakiwa na kumuona mtaani hapo ndipo Viongozi wa Chama cha Mapinduzi tutakapo dili na Jeshi la Polisi"NAPE NAUYE ASEMA
Imechapishwa na kuandikwa na Evance Willfredy
ALHAJI MANSOOR AAHIDI KUCHIMBA VISIMA VYA MAJI KATA YA PANGANI -KIBAHA
-
Mlezi wa Twarika lkadiriya (Islam) wa Mkoa wa Pwani Alhaji Mussa Mansour
ameahidi kuchimba visima viwili vya maji kwa wakazi wa Kata ya Pangani
iliyopo...
Saa 3 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni