Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Bongo Fleva Sam Wa Ukweli akiwaburudisha Wananchi wa Kiwangwa katika Kampeni ya Mgombea Ubunge kupitia CCM na ni Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Ridhiwani Kikwete.
Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa CCM akiwasili katika Viwanja vya Kata ya Kiwangwa katika jimbo la Chalinze kwania ya kuwaomba Wananchi Kura ili awe Mbunge wao.
Katibu wa Itikadi na Uwenezi Taifa Nape Nauye akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze Mjumbe wa Halmashauli kuu Taifa CCM Ridhiwani Kikwete hayupo pichani katika Viwanja vya Kata ya Kiwangwa.
Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa CCM Ridhiwani M.Kikwete akisaini kitabu cha Wageni alipowasili katika viwanja vya kata ya Kiwangwa ili kuwahutubia Wananchi
Wananchi wa Kata ya kiwangwa wakimsubili kwa hamu kubwa Mgombea wao wa Ubunge Jimbo la Chalinze Mjumbe wa NEC Ridhiwani M.Kikwete awasili.
Wazee wa Kata ya Kiwangwa wakimsikiliza Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Ridhiwan M.Kikwete katika kikao cha faraga baada ya kumaliza Mkutano wa Kampeni yake.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimajaro Mzee Kazidi akimnadi Mjumbe wa NEC Taifa Ridhiwani Kikwete katika Kampeni za Kuwania Ubunge katika jimbo la Chalinze.
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Ridhiwani Kikwete akiwa katika kikao cha faraga na Wazee wa kata ya Kiwangwa huku akiwa na Makada wa Chama cha Mapinduzi.
Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete juzi aliwahutubia wakazi wa Vijiji vya Bago,Mwetemo,Kiwangwa na kupata fulsa na kukutana na Wazee wa Vijiji hivyo na kuwaambi mambo ambayo amezamilia kuwafanyia pindi atakapopata nafasi ya kuwa Mbunge wao wa Jimbo la Chalinze.
Akiongea kwa Masikitiko makubwa pindi alipofika katika Vijiji hivi na kujionea hali mbaya ya kimaisha jinsi wanavyoishi Wanakijiji hawa Mjumbe wa NEC CCM Taifa Ridhiwani Kikwete
alisema kuwa atazitekeleza Changamoto zote ambazo ameambiwa na Viongozi wa Serikali za Vijiji hivyo na zingine ambazo amejionea mwenyewe.
Zifuatazo ni changamoto ambazo Mjumbe huyu alikutananazo pindi alivyozuru katika Vijiji hivi:
A/ELIMU:Nitahakikisha kuwa Madarasa yanajengwa na nyumba za Waalimu za kutosha ili Wanafunzi wapate Elimu nzuri na kusoma karibu kupunguza umbali na Waalimu wapate makazi ili wawe na moyo wa kuwafundisha Wanafunzi wapate fauru kupunguza kundi la vijana wasio na ajira.
B/AJIRA:Katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi nitahakikisha kuwa Vijana wa Vijiji hivi wanapata ajira kwa kuwashawishi Wawekezaji waje kuwekeza katika Vijiji hivi ambavyo wakazi wake wanajishughurisha na vilimo vya Matunda kama Mananasi,Machungwa,n.k ili waweze kufungua Viwanda vya Juisi ambavyo vitawasaidia Wananchi kuuza Matunda yao kwa bei nzuri na kupata kipato kizuri pia Vijana kuajiliwa katika Viwanda hivyo.
C/MIGOGORO:Katika Vijiji hivi nafahamu kuwa kuna Migogoro ya Ardhi ambayo ni baina ya Wafugaji na Wakulima.Nitahakikisha kuwa Migogoro naimaliza kwa kuwatengea Wakulima maeneo yao ya kilimo na Wafugaji maeneo yao ya kufugia Wanyama.
D/MICHEZO:Kwa kushirikiana na Serikali za Vijiji nitatekeleza suala zima la Michezo kwa kuwapa kipaumbele Vijana washiriki katika Michezo hasa kwa kuanzisha mashindano kama ya Mpira kwa Vijana wa Kiume na Mpira wa Pete kwa Wanawake.Natambua kuwa Michezo ni kujenga mwili,kufahamiana na watu,kujenga uhusiano mzuri na watu wa ndani na nje, Ntapenda kuwaona Vijana wakishirikiana kwa jambo hili kwani litawapunguzia kuepuka na makundi ya ajabu na kuiweka miili yao kujengeka kimazoezi
E/HUDUMA ZA JAMII:Kwa kutekeleza Ilani ya Chama changu cha Mapinduzi,nitawawekea Zahanati Ili Wananchi hasa Wanawake Wajawazito wapate huduma ya Kujifungua karibu na Kupunguza Vifo vyao,Nitawawekea Umeme kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo,na nitatekeleza kwa kuwawekea Barabara ambazo zitarahisisha shughuli katika Mendeleo ya Vijiji.
CCM Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!
Imetayalishwa na Evance Wilifredy
0 comments:
Chapisha Maoni