"TUTAKUPA KURA NDUGU YETU HATUTOKUANGUSHA"


Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani Kikwete akiwa na viongozi wa Kijiji cha Masugulu alipowasiri kwa nia ya kuwaomba kura Wananchi wa Kijiji hicho Kata ya Kiwangwa.Wananchi walimpokea kwa Shangwe mgombea huyo na kumuahidi hawatomuangusha watampa kura zote kwa sababu ni Ndugu yao,Mtoto wao,Kaka yao,na Kijana wao

 Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete akiwahutubia Wanakijiji wa kijiji cha Masugulu alipowatembelea kuwaomba ridhaa ya kuwa Mbunge wao mtarajiwa kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Mjumbe huyu wa NEC Taifa Ridhiwani aliwaahidi Wanakijiji kuwapatia Maendeleo ambapo atashirikiana na Mh.Diwani pamoja na viongozi wa Serikali ya Kijiji katika kufanikisha ilo.
Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete akiwasiri katika kijiji cha Mwetemo huku akilakiwa na umati wa Wanakijiji wa Kijijini hapo alipowatembelea katika moja ya Kampeni zake za kuwaomba ridhaa Wananchi wa Jimbo la Chalinze awe Mbunge wao.Wananchi walifurahi sana walipomuona Mbunge wao mtarajiwa alipowatembelea.
Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani Kikwete akiwa pamoja na viongozi wa Kijiji cha Mwetemo katika Kampeni zilizofanyika katika Kijiji hicho kilichopo kata ya Kiwangwa jimbo la Chalinze.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mwetemo nd.Hosein Kizenga akitoa ufafanuzi juu ya changamoto zinazowakabili katika kijiji hicho kwa Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi Mjumbe wa NEC Taifa Ridhiwani M.Kikwete hayupo pichani katika Jimbo la Chalinze.
Makada wa Chama cha Mapinduzi wakicheza Muziki ambao uliokuwa ukitumbuizwa na Msanii wa kizazi kipya Sam wa Ukweli hayupo pichani katika Kijiji cha Msinune katika Kampeni zinazoendelea za mgombea Ubunge kupitia CCM Mjumbe wa NEC Taifa Ridhiwani M.Kikwete katika Jimbo la Chalinze 
Wananchi wa kijiji cha Msinune wakimsikiliza kwa makini Mgombea Ubunge wa jimbo la Chalinze Mjumbe wa NEC Taifa Ridhiwani Kikwete alipokuwa akiwaeleza sababu gani zilizomfanya afike kijijini hapo katika kampeni zake zinazoendelea katika jimbo hilo.
Bibi anayejulikana kwa jina la Bi Anazina Mrisho Mfaume ambaye alitembelewa na Mgombea kiti cha Ubunge kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa  Ridhiwan M.Kikwete kulia katika kijiji cha Msinune kata ya Kiwangwa katika jimbo la chalinze alipodhuru kuwaomba Wananchi kura.
 Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Ridhiwani M.Kikwete akiwa na mtoto Hamisi Juma ambaye alimfuata nd.Ridhiwan kumtaka ampatie kofia ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kijiji cha Msinune kata ya Kiwangwa katika moja ya kampeni zake za kuomba kura kwa wananchi ila baadae Mgombea huya aliweza kumpatia kofia mtoto huyu.


Hii ni Ofisi katika kijiji cha Msinune kata ya Kiwangwa ambayo inashugurikia masuara ya Ardhi na kuondoa migogoro ya Ardhi ambayo imekuwa ikiwaandama Wafugaji na Wakulima katika Mikoa ya Tanzania.
Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete akisalimiana na wazee wa kijiji cha Msinune kata ya Kiwangwa alipowatembelea kuwaomba kula Wananchi wa hapo na kuwaahidi ahadi kemkem ambazo nd.Ridhiwani aliwaahidi kuwatekelezea endapo watampa nafasi ya kuwa Mbunge wao.

Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Ridhiwani M.Kikwete akiongea na Katibu wa CCM wa Wilaya Mkoa wa Tanga Mjini Mh.Lucia Mwilu katika kijiji cha Masugulu kata ya Kiwangwa katika kampeni za kuwania Ubunge jimbo la Chalinze.
''TUTAKUPA KURA NDUGU YETU HATUTOKUANGUSHA"Huo ndio msemo na  kauli waliozitoa Wananchi wa Vijiji vya Masugulu,Mwetemo,Msinune vya Kata ya Kiwangwa ambapo Mjumbe wa Halmashauri CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete alipofanya Ziara katika Vijiji hivyo kwa nia ya kuomba Dhamanaya kuwa Mbunge wao kupitia jimbo la Chalinze,

Moja ya mambo ambayo ndugu Ridhiwani Kikwete aliwaahidi Wananchi wa vijiji hivi kuwa atawatekelezea endapo watamchagua kuwa Mbunge wao wa Jimbo la Chalinze ni kama ifuatavyo:

1.ELIMU'
Mjumbe Halmashauri kuu Ccm taifa aliwaambia Wananchi wa Vijiji hivi kuwa Mazingira mazuri ya Shule ndio yaliyomfanya asome vizuri mpaka kufika hapa alipo,Ataboresha Mazingira ya Shule za Msingi na Sekondari kwa kuchimba Vyoo na kuongeza Madarasa kwa shule ambazo zina Madarasa pungufu.

Atawezesha kwa kila Shule zenye Waalimu pungufu kwa kushirikiana na Serikali za Kijiji pamoja na Diwani kuhakikisha Waalimu wanakuwepo wa kutosha na wenye uwezo wa kufundisha ili watoto waweze kupata elimu bora.Bila kubolesha Mazingira ya Shule zetu,tutaongeza wimbi la Watoto wa mitaani,umasikini pamoja na Kudhorotesha  Uchumi wa Vijiji vyetu kuwa nyuma Kimaendeleo.

Pia aliahidi kuwepo kwa nyumba za waalimu za kutosha kwa kila Shule ambazo zitapunguza Waalimu kukaa mbali na kuchelewa katika kazi zao na kusababisha kufika Shuleni masaa yamepita na kusababisha wanafunzi kutokumaliza silabasi za masomo yao na Wanafunzi kufeli Masomo.

2.UMEME"
Haikuishia hapo,Mjumbe huyu wa Nec vilevile aliwaahidi Wanakijiji kuwa ataweza kuweka Umeme kwa kufuata Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kila Kijiji ila kwa kuwasihi Wanavijiji waweze kuangaika ili waweze kuweka bati Nyumba zao kwanza ili kuondoa hali za hatari kwa kuunguliwa Nyumba zao.

Ataweza kuweka Umeme Mashuleni ili Wanafunzi waweze pata Elimu Bora ambayo itawezesha kuondoa tatizo la Umasikini ambalo ni janga kubwa kwa Taifa letu.

3.MIGOGORO YA ARDHI"
Akizungumzia suala la Migogoro ya Ardhi nchini baina ya Wafugaji na Wakulima Mjumbe huyu wa NEC Taifa alisema,Migogoro ya aina hii imekuwa mingi Nchini kutokana na kutokuwepo Mazingira mazuri ya kuwatengea Wafugaji Maeneo ya Kulishia Mifugo yao na kusababisha Mifugo yao kuingia katika Mashamba ya Wakulima na kusababisha Migogoro ambayo haina Msingi na Kurudisha Maendeleo ya Nchi na Wanakijiji wenyewe nyuma.

Alisema kuwa atahakikisha chini ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi kuwa ataweka Miundombinu ya Marisho ya Wafugaji na kuwahamasisha wawe na maeneo ya Ufugaji Maalumu ambayo yatakuwa nje ya Miji na kusababisha kupungua kwa Migogoro hii.

4.VIWANDA"
Kutokana na Vijiji hivi kuwa na Vilimo cha Matunda kama Mananasi,Machungwa,Maembe,na n.k  ataviwezesha Vijiji hivi katika Jimbo hili la la Chalinze kwa kuwatafuta wawekezaji ili waweze kuweka viwanda katika Vijiji hivi ili Wanakijiji waweze kuuza Mazao yao kwa kupata faida kubwa ambapo wataweza kuwa na maisha mazuri na kuliletea jimbo Maendeleo.

Vilevile Mjumbe huyu wa Halmashauri kuu CCM Taifa ambaye anaonekana ni kuwa ni Kipenzi cha vijana wengi katika jimbo hili la Chalinze alisema kuwa pia kutokana na kuwepo kwa Viwanda hivi vitasababisha kwa Vijana kupata Ajira na kujiwezesha wenyewe katika kuinua Uchumi wao wa kimaisha na kuweza kupiga hatua na kupunguza Makundi ya Vijana wasio na Ajira.

5.AFYA"
Aliongeza kwa kuwaambia kuwa anafahamu suala zima la wanawake wajawazito kupata Tabu na shida ya kujifungua pindi inavyofika wakati wa kujifungua kutokana na Zahanati kuwa mbali na Vijiji.Kwa kushirikiana na Serikali za Vijiji atahakikisha kila Kijiji kinakuwa na Zahanati yake yenye Wauguzi walio na Elimu ya kutosha."Naomba Mnipe kura zenu wananchi ili niwe Mbunge wenu na niwafanyie yale yote nilio waahidi kwa kushirikiana na Viongozi wenzangu wa Kijiji"

              Baada ya kumaliza mkutano wake na Wanavijiji hawa ndipo zilifuata vigeregere na vifijo toka kwa wanavijiji huku wakimuimbia Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa "TUTAKUPA KURA ZETU NDUGU YETU NA WALA HATUTOKUANGUSHA"

                    CCM Ooooooyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.........................................
                                          Imeandikwa na kuchapishwa  na Evance Willfredy
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List