KAMPENI ZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE ZAPAMBA MOTO

Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Ridhiwani M.Kikwete akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Mh.Mwinshehe S.Mlao katika kampeni ya kuwania kiti cha Ubunge katika jimbo la Chalinze katika kijiji cha UBENA
Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Ridhiwani M.Kikwete akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Ubena katika moja ya kampeni zake katika Jimbo la Chalinze.
Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa CCM Ridhiwani Kikwete akiwasiri huku akicheza mziki katika moja ya kampeni zake alizofanya katika Jimbo la chalinze.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Samu wa ukweli akitumbuiza katika kampeni akimnadi mgombea kiti cha Ubunge kupitia chama cha CCM Mjumbe wa NEC Taifa Ridhiwani M.Kikwete katika jimbo la Chalinze mapema leo.
 Nd.Ridhiwani M.Kikwete akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika kijiji cha Mdaura.
Ndugu Ridhiwani M. Kikwete akisalimiana na wakazi wa Mdaura leo katika kampeni za kuwania Ubunge wa jimbo la Chalinze.Wananchi wengi walijitokeza katika kampeni hii.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Afsa Kazinja nae hakuwa nyuma katika kuhakikisha Kampeni za kumnadi mgombea Ubunge kupitia Chama cha mapinduzi CCM Nd.Ridhiwan M.Kikwete analinyakua jimbo la Chalinze katika kijiji cha Ubena kata ya Ubena iliyofanyika leo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dokii nae hakuwa mbali katika kuhakikisha ipasavyo anamnadi Mgombea wa kiti cha Ubunge kupitia chama cha CCM Mjumbe wa NEC CCM Taifa Ridhiwan M.Kikwete kijiji cha Ubena kata ya Ubena.

Mgombea kiti cha Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi CCM Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete ameendelea kufanya kampeni za uchaguzi jimboni kwake huku akinadi sera za chama chake.Akiwa katika kijiji cha mdaura huku umati wa watu ukiwa mkubwa na kupokewa na wananchi waliokuwa na furaha huku wakimuimbia nyimbo na ngoma, Ridhiwani aliwaambia wananchi kuwa endapo watampa ridhaa ya kuwa Mbunge wao atawafanyia mambo yafuatayo:

1.ELIMU
Kuhusu suala la Elimu,Ridhiwani aliwahakikishia wananchi wa Ubena na Mdaura kuwa ataweza kujenga Shule nyingi na kuwawezesha wananchi wa vijiji hivi watoto wao kupata Elimu Bora na kuondoa wingu la umasikini linalowazunguka wananchi wa vijiji hivi.Vilevile ataongez madarasa katika shule ambazo zina upungufu wa madarasa pamoja na kuwaongeza waalimu wawe wengi ili kuondoa tatizo la upungufu wa waalimu.

2.MAJI
Ridhiwani aliwahakukushia wananchi wa vijiji hivi kuwa atashirikiana na Serikali za Vijiji kuhakikisha wananchi wanapata Maji yaliyo salama kwa kuweka mabomba na kuchimba visima ambavyo vitasaidia kuwepo kwa maji salama na kupunguza idadi ya magonjwa ya mripuko yanayotokana na maji yaliyo si salama.

3.AFYA
.Ridhiwani M.Kikwete aliwasisitizia Wananchi wa vijiji hivi vya Ubena na Mdaura kuwa atawawezesha kwa kupata Afya iliyo Bora kwa kuwajengea Zahanati za kisasa kwa kushirikiana na Serikali za vijiji na Ilani ya chama cha mapinduzi na kuondoa matatizo ya wanawake wajawazito kufia njiani pindi wanapopelekwa zahanati zilizo mbali.

4.BARABARA
Mjumbe wa NEC CCM Taifa.Ridhiwani aliwaomba wananchi wampe Ridhaa ili awe Mbunge wao ili aweze kuwajengea Barabara ambazo zitaunganisha vijiji baina ya vijiji na mikoa baina ya mikoa ili kurahisisha shughuri za kiuchumi na wananchi kupata Fursa ya kupeleka bidhaa zao katika sehemu nyingine bila buguza zozote zile.

5.MICHEZO
Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete aliwaambia vijana wa vijiji hivi kuwa ataanzisha kombe la diwani cup ili kuwakutanisha vijana kwa pamoja ili kujenga ushirikiano ulio imara na kutanua wigo la vijana kufahamiana".Michezo ni afya,upendo,na kufahamiana,hivyo hatuna budi kuwakutanisha vijana wawe pamoja ka kujenga ushirikiano ulio bora''

6.AJIRA
Vijana wa vijiji vya Ubena na mdaura wameambiwa kuwa,wakimpa nafasi ya kuwa Mbunge wao watawezeshwa kupata mikopo na kujiajiri wenyewe kwa kuungana katika vikundi mbalimbali.
"vijana watapata Fursa ya kupata mikopo iliyo na liba nafuu na kuweza kujiajiri wenyewe ili kujiinua katika hali ya uchumi na kuwa na maisha bora"
                                   CCM Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!
                                          Imetayalishwa na Evance Willfredy
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List