Askari Polisi ni watu ambao kila kukicha wanapata Tuhuma na Kashfa za kulichafua jeshi la Polisi la Tanzania kutokana na Mazingira magumu ya wanayofanyia kazi.Tuhuma nyingi sana ambazo zinawalenga Askari Polisi kama Kupola vitu vya Raia,Kupokea Rushwa,Huonevu,Mafisadi,Wanyonyaji,Wadidimizaji N.k.
Hizi ni Miongoni mwa Kashfa ambazo huwa wanapewa Askari hawa wa Jeshi la Polisi.
Watanzania Askari Polisi tumewaweka ni watu wa ajabu huku tukisahau ya kuwa ni Binadamu ambao wanaweza kukosea kama Binadamu wengine.Sote tunatambua Askari Polisi ni watu wanaolinda Mali za Wananchi pamoja na Usalama wao kutokana na sisi wenyewe Wananchi ndio tunaowafanya Askari wawe na Uwajibu huo kutokana na Makosa tunayoyafanya dhidi ya Binadamu wenzetu kunyume na Sheria.
Wiki 2 zilizopita nilikuwa katika Maeneo ya Mwananyamala Kisiwani karibu na Ofisi ya TOT,kulikuwa na kundi la Vijana ambao walikuwa wameambatana na Wazazi wao wakimlalamikia Askari Polisi wa kituo cha Oysterbay Inspekta Jacob Swai.Walikuwa wakimtuhumu kwa Kashfa za Kuwaonea,Kuwapora vitu kama simu za mkononi,Kuingia katika Vyumba vya Wapangaji bila ya ridhaa ya wenyenavyo,Kuwakamata pasipo na Makosa,Kuwafikisha Mahakamani pasipo na vidhibiti pamoja na Kuwapiga wao pamoja na Wazazi wao.
Hivi huyu Askari ni Chizi,Mwehu,Jeshi la baba yake,au?Ni Maswali ambayo tunayopaswa kujiuliza Wananchi.Cha ajabu ni hivi,Wale Vijana ambao waliokuwa wakimlalamikia Inspekta Swai wa Jeshi la Polisi ukiwaangalia Sura zao Dhahiri wanaonekana ni Wanauza na kutumia Madawa ya Kulevya,Mateja,Wezi,n Wakabaji kiasi ambacho hata ungelikuwa ni wewe ndiye Operesheni Ofisa kama Inspekta Swai ungeliwakamata kutokana na tabia zao na muonekano wao.
Inspekta Jacob Swai ni Operesheni Ofisa wa Mkoa wa Kinondoni ambaye anastahiri pongezi za kipekee Kutokana na Kukabiliana na Waalifu katika Mazingira Magumu sana ambayo Mwisho wa Siku ni kupewa Kashfa na Kuchukiwa.
Mtaa huu wa Mwananyamala Kisiwani ni Mtaa ambao vijana wengi hawana Shughuri za Kufanya kiasi cha kufikia Kujishughurisha na Uharifu kama Kuuza Madawa ya Kulevya MF;bangi,kokeini na mwisho wa siku kujikuta wakiyatumia wenyewe,Kuiba,Kuvunja,na Kutishia Usalama wa Raia.
Uharifu wote huu fikiria Mwananchi ungelikuwa Mtaani kwako na mnafika Polisi na kuwaeleza Askari Uharifu unavyofanyika Mtaani kwako na Vijana,Ungelichukuliaje Jeshi la Polisi kama halichukui hatua na wajibu wa kuwashughurikia Vijana hawa ambao wanafanya Uharifu?
Mfano Uharifu wa kundi la Mbwa Mwitu katika Mkoa wa Temeke uliwaathiri Wananchi wangapi,Mkoa wa Temeke hali yake ilikuwaje?Haya mambo tunatakiwa kujifunza na yasiwe yanajirudia rudia kutokana na kuwafuga Waalifu alafu mwisho wa siku wanatuzuru sisi wenyewekama kundi hili la Mbwa Mwitu.
Inspecta huyu ni mfano wa kuigwa kwa maaskari wenzie Jinsi alivyopambana na waarifu wa Mkoa wa Kinondoni na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza Uharifu huko Mwananyamala na sehemu zingine za Mkoa huu.Kwa sasa pako shwari tofauti na kipindi cha nyuma cha roba za mbao.
Wananchi tuache kulipaka tope Jeshi la polisi hasa watendaji wake huku tukisahau kushirikiana nalo katika kuwafichua waalifu na kubaki na kubaki kulituhumu kwa Kashfa rukuki ambazo hazina msingi.
Tuwaache wafanye kazi kwa kushirikiana na nyinyi katika kuhakikisha wanatokomeza Uharifu nchni mwetu.
Pongezi kwa Jeshi la Polisi,Pongezi kwa Inspekta Swai kwa kukabiliana na wahalifu azidi kufanya kazi ya kiserikali bila kujari matatizo atakayokumbana nayo.
Imeandikwa na Kuchapishwa na Evance Willfredy
KISARAWE KUKATA KEKI YA BIRTHDAY YA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
-
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti akizungumza kwenye mkutano na
Waandishi wa Habari hawapo pichani kulia kwake ni Hakimu Mkazi Mkuu
Mfawidhi wa Maha...
Siku 1 iliyopita
0 comments:
Chapisha Maoni