Mangula asubiri Ukawa wajibu hoja za kuhongwa mabilioni

Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara, Phillip Mangula, amesema vyama vinavyounda Umoja wa Katiba Tanzania (Ukawa), vinasubiriwa kujibu tuhuma zinazokabili umoja huo, za kuhongwa mabilioni ya Shilingi, ili wasihudhurie katika Bunge Maalumu la Katiba, linalotarajiwa kuanza mwanzoni mwa Agosti mwaka huu.

Akasema Baraza la Taifa la Vyama vya Siasa, lenye vyama vyote 22 , litakutana hivi karibuni kujadili hatma ya Bunge hilo Maalumu la Katiba ambapo baadhi ya masuala yanayotarajiwa kujiri, ni tuhuma hizo za kuhongwa kwa Ukawa na baadhi ya mashirika ya kigeni.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa jana, Mangula alisema Juni 8, mwaka huu, vyama vyenye wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano, vilikutana ili kutafakari mwenendo wa vyama na athari zake kwa hali ya siasa nchini, lakini kukosekana kwa vyama vya Chadema na CUF, kulisababisha mkutano huo usimalizike vyema.

Kikao hicho kiliandaliwa na Kamati ya Ufundi ya Kituo cha Demokrasia nchini (TCD). Vyama vinavyounda TCD ni sita tu, ambavyo ni CCM, Chadema, CUF, NCCRMageuzi, TLP na UDP.

Vyama hivyo ndivyo vyenye wabunge na chama cha UPDP kinawakilisha vyama visivyokuwa na wabunge. Alisema madhumuni ya kikao hicho cha TCD, yalikuwa kujua matatizo yaliyowafanya baadhi ya washiriki wa Bunge hilo la Katiba, kulisusia na kutoka nje ya ukumbi.

Alisema wajumbe wa kikao hicho, walishindwa kukamilisha azma yao, kutokana na kutokuwepo kwa wawakilishi wa vyama vya Chadema na CUF.

“Baadhi ya wajumbe wa TCD walitaka kujua kauli ya wana Ukawa waliotoka bungeni na baadaye kurejea na kuendelea na Bunge, wakiungana na wawakilishi wa vyama 16, kati ya 22, vilivyobaki bungeni, wakiviacha vyama vitatu vya Chadema, CUF na NCCR nje,” alisema Mangula.

Alisema wajumbe wengine, walitaka kusikia kauli ya Ukawa, kuhusu tuhuma nzito, zilizotolewa kwenye vyombo vya habari, vilivyodai kuwa yapo mashirika mawili ya kigeni, yanayofadhili wajumbe wa Ukawa, kuacha kuhudhuria vikao vya Bunge Maalumu.

Mabilioni “Taasisi hizo za mataifa ya nje, ndizo zenye mfuko wa fedha watakazolipwa Ukawa Sh 450,000 kila siku kila mmoja kwa wasioingia kwenye Bunge la Katiba litakaloanza Agosti. “Ukawa ilipokea Shilingi bilioni 1.7 Machi mwaka huu na baadaye Ukawa ilipokea Sh milioni 380. Kuna ahadi ya Ukawa kupatiwa kiasi kingine cha Sh bilioni 3.2 baada ya kupeleka mrejesho wa matumizi ya mgao wa kwanza,” alidai Mangula.

Alisema: “Kwa kuwa wahusika wakuu wa tuhuma hizi hawakuwemo kwenye hicho kikao cha TCD ili kutoa ufafanuzi, wajumbe tumekubaliana kuitisha kikao cha Baraza la Taifa la Vyama vya Siasa linalojumuisha vyama vyote 22 vyenye usajili wa kudumu ili kuendelea kutafakari hatma ya mchakato katika awamu ya pili ya Bunge.”

Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara, Phillip
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List