Baadhi ya Maofisa Habari Mawasiliano wa Wizara za Serikali, wakielekea katika Ukumbi wa Mkutano wa Bunge mjini Dodoma, leo. Maafisa hao wamefanya ziara Bungeni hapo ili kuona shughuli za Bunge.
Baadhi ya Maafisa Habari Mawasiliano Serikalini wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene (wa nne kutoka kushoto mstari wa mbele). Wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge leo kuangalia shughuli za Bunge mjini Dodoma.
Baadhi ya Maafisa Habari Mawasiliano Serikalini wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Aggrey Mwanri akiwakilisha hati mezani kuhusu Taarifa ya Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa na Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha,2010/2011.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Pereira Silima akiwasilisha azimio la Bunge la Kujiunga na Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia Vitendo vya Ugaidi wa Kutumia Nyuklia. Azimio hilo limeungwa mkono leo katika mkutano wa kumi kikao cha nane.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru Kawambwa (kulia) akiongea na James Mbatia (Kushoto)- katika viwanja vya Bunge leo. Baada ya Spika Anne Makinda(hayupo pichani) kutangaza rasmi Mitala ya Elimu inayotumika ni halali na ipo. (Pichani katikati) ni Charles Mwijage (Muleba Kaskazini).
Mwenyekiti wa Bunge Mussa Zungu Azzan akifafanua kanuni mbalimbali Bungeni leo.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe(kushoto) akiongea na Joshua Nassari(Arumeru Mashariki) ndani ya ukumbi wa Bunge. Picha Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.
Blogger Comment