Mfungaji bao la Argentina ,Lionel Messi
Lionel Messi alifunga bao la pekee na la ushindi katika dakika ya mwisho ya mechi baina ya Argentina na Iran ya kundi G.
Mechi hii ilikuwa na kila dalili ya kuishia sare tasa sawa na ile ya kwanza kati ya Iran na Nigeria ambapo vijana wa Carlos Queiroz walizima kila dalili ya shambulizi kutoka kwa Argentina.
Kocha wa Argentina Alejandro Sabella alimpiga pambaja Messi baada ya kipenga cha kukamilika kwa mechi hiyo kupulizwa .
Argentina walikuwa wameshinda mechi yao ya awali dhidi ya Bosnia Hercegovina.
Irana kwa upande wao walikuwa wamedhibiti Nigeria na wakajizolea alama moja kutokana na sare tasa .
Licha ya juhudi zake Jala Hosseini Ashkan Dejagah mechi hiyo ilikuwa imesalia kuwa Argentina wanashambulia nao Iran wakihimili mashambulizi yote.
Javier Mascherano, Fernando Gago , Angel Di Maria, Pablo Zabaleta na Marcos Rojo wote walipata nafasi ya kushambulia Iran lakini mwishowe ilikuwa ni Messi aliyewapa tikiti ya mkondo wa pili.
Argentina licha ya kuwa wamesalia na mechi moja dhidi ya Nigeria sasa wananafasi nzuri ya kuwania kombe la dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1986.
Blogger Comment