Bondia wa kike,Lulu Kayege akiwa katika pozi bondia huyo anaenolewa
katika Kambi ya Ilala na Makocha wazowefu wa mchezo wa Masumbwi Nchini
Habibu Kinyogoli 'Masta, Rajabu Mhamila 'Super D' na Kondo Nassoro kwa
sasa yupo fiti kwa ajili ya masindano mbalimbali nchiniwww,superdboxingcoach.
blogspot.com
Na Mwandishi Wetu
Ukizungumzia mchezo wa masumbwi ulivyompatia hamasa mpaka
kuanza mazoezi katika kambi ya ilala ya mchezo wa masumbwi bondia Lulu Kayage anasema mchezo anaupenda na pia
unamjenga kiafya na ki mwili kwani amekuwa akishiriki mazoezi tangia mwaka 2012
mwezi April na maendeleo yake ni mazuri akiwa chini ya
uwangalizi wa makocha wake hawo
Bondia huyo wa kike aliyezaliwa 1990 anamatarajio makubwa ya kuwa ingwa wa dunia katika masumbwi ususani upande wa wanawake
bondia
huyo anaye vutiwa na uchezaji wa mkongwe wa masumbwi nchini Rashidi
Matumla 'Snake Man' ambapo kwa nje anavutiwa na mabondia toafauti
ambapo mmoja wapo ni Mbunge wa Filpino Manny Paquaio na bondia
asiyepigika ambaye kwa sasa anatumikia kifingo cha siku 90 kwa kosa la
kumshambulia aliyekuwa mpenzi wake na mama watoto wake
Katika mazoezi anayofanya na kambi ya Ilala ambayo wanawake wapo
wawili ambapo anaendelea kujisikia faraja kwa kuwa wapo katika mazoezi
pamoja kama ndugu na nidhamu ya ali ya juu iliyopo hapo katika kambi
hiyo
aliwataka wanawake wajitokeze katika
mchezo wa masumbwi kwani ni mchezo kama michezo mingine ambapo ata
ukiangalia mchezo watu wanapopigana wakimaliza wanakubatiana kwa furaha
ni kwa ajili ya kutambua mchezo wa masumbwi si uadui bali ni mchezo
Vikwazo ambavyo amewai kukutana navyo
ni pamoja na kukatishwa tamaa kwa watu ambao awapendi michezo kwani
wanasema mwanamke mzima unacheza ngumi uogopi kutolewa manundu kuaribiwa
sura ehee uzuri wote huo hizo ni sehemu tu za watu wasiopenda michezo
kwani kuna vikwazo
vingi ambavyo tuna vipata mabondia wa kike
kwa
mara ya kwanza nilipotokea kwenye magazeti tu watu walinifata na
kunishauli niachane na mchezo lakini kwa sasa nimeshaiva na nipo tayali
kwa mapambano mbalimbali yatakayojitokeza
kwa kuwa mimi ni bondia bora pekee wa kike nchini na
ninaetoka katika kambi bora kabisa ya mchezo wa masumbwi nchini naisi
cheche zangu mtaanza kuziona mwazi agost kwa kuwa kwa sasa nipo kwenye
mazoezi makari ambayo yananipa uwezo wa ali ya juu katika masumbwi
Aliongeza kuwa kwa kufundishwa na kocha wa kimataifa
Super D anaefundisha mafundisho hayo kupitia DVD zake ambazo
amechanganya na clips za mabondia mabingwa wa dunia akiwemo Manny
Paquaio,floyd Mayweather, Roy Jones, Mohamedi Ali, Mike Taysoni na
wengine ameziona na kuzifanyia kazi ambapo kwa sasa anajua mbinu za
Ndani na nje ya nchi kutokana na Supe D kumpatia uwezo wa kina katika
maswala ya mchezo wa Masumbwi Duniani
Katika mchezo uhu siwezi kukata tamaa katika mazoezi
na nawambia mashabiki wa mchezo wa masumbwi watarajie mafanikio yangu
katika masumbwi
0 comments:
Chapisha Maoni