Viingilio kwa mechi ya Taifa Stars na Msumbiji itakayochezwa keshokutwa (Jumapili) Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ni sh. 7,000 na sh. 30,000 kwa viti maalumu 4,500 tu.
Kuanzia kesho asubuhi (Jumamosi) tiketi za kielektroniki zitauzwa pia katika magari maalumu kwenye vituo vya Buguruni Shell, Dar Live Mbagala, Ferry Magogoni, Kigamboni, OilCom Chang’ombe, OilCom Ubungo, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa (Kariakoo), TCC Club Chang’ombe na Uwanja wa Taifa.
Aidha tiketi zinapatikana kupitia M-PESA kwa kupiga *150*00# kisha bonyeza 4, bonyeza tena 4 kisha weka namba ya kampuni 173399 kisha ingiza 7000 kama namba ya kumbukumbu ya malipo, kisha andika tena 7000 kwenye weka kiasi, kasha weka namba ya siri na baadaye bonyeza 1 kukubali.
Utapokea ujumbe wenye orodha ya vituo vya MaxMalipo vya kuchukua tiketi ukiwa na namba ya uhakiki wa malipo yako.
Vituo vya MaxMalipo vya kuchukulia tiketi ni mgahawa wa Steers uliopo mtaa wa Samora/Ohio, maduka makubwa ya Uchumi Supermarket (Quality Centre, Tabata Segerea na kituo cha daladala Makumbusho), Sheer Illussions (Millennium Tower na Mlimani City), maduka makubwa ya TSN Supermarket (City Centre, Kibo Tegeta na Upanga).
Vodashop (Ubungo na Mill Pamba), Shop Mwenge (Born to Shine), Puma Petrol Station (Mwenge na Uwanja wa Ndege), Engen Petrol Station (Mbezi Beach), Big Bon Petrol Station (Kariakoo, Sinza Mori, Mbagala na Temeke), YMCA (Posta Mpya), City Sports Lounge (Posta), Uwanja wa Taifa) na Uwanja wa Karume.
SEMINA ELEKEZI AIRTEL RISING STARS
Semina elekezi ya michuano ya Airtel Rising Stars kwa mikoa sita inafanyika kesho (Julai 19 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Washiriki wa semina hiyo ni kutoka mikoa ya Mbeya (Katibu na mwakilishi wa wanawake), Mwanza (Katibu na mwakilishi wa wanawake), Morogoro (Katibu), Ilala (Katibu na mwakilishi wa wanawake).
Temeke (Katibu na mwakilishi wa wanawake), Kinondoni (Katibu na mwakilishi wa wanawake), Dar es Salaam (Mwenyekiti na Katibu), na Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) kitakachowakilishwa na mwakilishi wa wanawake.
Washiriki wengine katika semina hiyo ambayo mgeni rasmi atakuwa Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine ni wajumbe wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana ya TFF.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Chapisha Maoni