Alejandro Sabella, kocha wa timu ya taifa ya Argentina amemwelezea winga wa Uholanzi Arjen Robben kama mchezaji hodari kwenye michuano ya kombe la dunia lakini amesema Messi bado ni mchezaji bora
Alipozungumza na waandishi wa habari jana jumanne, alichukuwa muda kumlinganisha Robben, Neymar na Messi lakini bado alikiri kuwa Messi ni mchezaji bora.
"Nadhani ni mchezaji bora, muhimu sana kwa Uholanzi kama alivyo Neymar kwa Brazil lakini Messi ni bora zaidi yao," alisema Sabella
"Ni mchezaji hatari sana, hivyo tunapaswa kuwa makini nae sana. Akiwa kwenye kasi, ni ngumu sana kuuchukua mpira," alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni