Luis Suarez ahamia Barcelona

Liverpool imekubali kumuuza mshambulizi wake Luis Suarez kwa Barcelona kwa kima cha pauni milioni 75.
Mchezaji huyo wa Uruguay mwenye umri wa miaka , 27, ambaye amepigwa marufuku ya miezi miinne kwa kumuuma mchezaji mwenzake wa Italy, Giorgio Chiellini wakati wa mechi yao katika kombe la dunia, atasaini mkataba wa miaka mitano.

"Luis ana kipaji cha kipekee, na ninamshukuru kwa alivyotuwakilisha,'' alisema meneja wa Liverpool Brendan Rodgers.Suarez, ambaye aliingiza mabao, 31 katika ligi ya premier msimu uliopita, atasafiri kwenda Uhispania wiki ijayo kwa uchunguzi wa kimatibabu.
Suarez anasema kuwa yeye pamoja na familia yake, daima watakuwa mashabiki wa Liverpool.
Suarez amepigwa marufuku kwa miezi minne kutocheza kimataifa
Suarez alikuwa mfungaji mabao mengi zaidi katika msimu uliopita na mshindi wa tuzo la mchezaji bora . Alitia saini mkataba na Liverpool alipotoka Ajax mwaka 2011 kwa pauni 22.7.
Alikuwa amesalia na miaka minne katika mkataba wake.
Hatua ya Suarez kuhamia Barcelona inampeleka karibu na mkewe pamoja na familia yake.
"Ni kwa majonzi mengi nimeamua kuondoka Liverpool, kwa maisha mapya nchini Uhispania na cha mno ni kwamba nimefurahishwa sana na mashabiki, '' alisema Suarez
"Ninatumai nyote mtaelewa uamuzi wangu. Klabu hii ilinifanyia kila nilichokitaka, lakini kucheza na kuishi uhispania, ilikuwa ndoto yangu kubwa. Muda huu uko sawa sana kwangu. ''

"Ninamtakia Brendan Rodgers na kikosi chake kila la heri na mustabali mwema. Klabu hiyo iko chini ya usimamizi mzuri na pia natumai watafanikiwa msimu ujao.''
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List