Picha ya Pamoja ya Semina ya siku moja ya Makatibu tawala Mikoa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Charles Pallangyo
Dar es salaam
KATIBU MKUU wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Charles Pallangyo,
emesema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha inamaliza tatizo la taka
ngumu mijini na vitongoji vyake.
Akizungumza katika semina ya siku moja ya MakatibuTawala wa Mikoa
iliyofanyika katika Hoteli ya jijini Dar Es Salaam,Pallangyo alisema,
Serikali imejipanga kumaliza tatizo hilo kuanzia katika ngazi ya
serikalii za mitaa hadi Mkoa.
katika kampeni ya kumaliza tatizo la uchafu, hususani katika miji,
kwani taka ngumu limekuwa tatizo sugu, hivyo tunafanya mikakati
mikubwa kuelekeza nguvu kuanzia ngazi ya jamii hadi juu ngazi za juu
Aidha Katibu Mkuu huyo alisema, lengo la kuandaa semina hiyo ni
kupanga mikakati ya kuhakikisha mazingira ya usafi yanazingatiwa,
katika jamii ili kuhepukana na vifo vinavyotokana na magonjwa ya
milipuko katibu mkuu wizara ya afya na ustawi wa jamii Charles pallagyo
Eliya Ntandu katibu tawala mkoa wa morogoro amesema lengo la serikali
ni kushirikiana pamoja na wanachi, secta binafsi,pamoja na wakandarasi,
kuzibiti mazingira na utupaji ovyo taka ngumu ambapo usimamizi huo
utasimamiwa na makatibu tawala wa kila mkoa
Wadau wa mazingira nchini pamoja na makatibu kutoka mikoa mbalimbali
waliudhuria semina hiyo wakisema kuwa nchini kumekuwa na tatizo kubwa
la usafi wa mazingira hivi sasa wizara imejipanga na kuweka mikakati
bora ya udhibiti na uchafuzi wa mazingira kwa kushirikisha wananchi
Pamoja na jitihada za serikari kupambana na usafi wa mazingira
wamebaini ipo haja ya kushirikisha wananchi pamoja na kutoa elimu ya
usafi wa mazingira ili kuepusha vifo na magonjwa ya mlipukoyanayotokana na uchafu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Charles Pallangyo
Mdau wa afya akichangia mada jinsi ya kuboresha usafi wa mazingira
ROBERT NTALENGA(mkurugenzi mwezeshaji wa Baraza la Mazingira Tanzania)
Picha ya Pamoja ya Semina ya siku moja ya Makatibu tawala Mikoa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Charles Pallangyo
Eliya Ntandu katibu tawala mkoa wa morogoro
Wakiwa wanasikiliza maelezo kwa Makini ndani ya Semina.
mwisho
0 comments:
Chapisha Maoni