Mafundi Gereji pamoja na wafanyabiashara mbalimbali walikuwepo eneo la Tegeta Kibaoni Magereji wameiomba Serikali iwasaidie kuendelea kubaki eneo waliopo ili waendelee kufanya kazi zao kwakuwa eneo ilo walipewa na Uongozi wa Serikali mwaka 2006 chini ya Mkuu wa Mkoa,Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi aliyekuwepo wakati huo katika Halmashauri ya Kinondoni Jijini Dar es salaam wakati huo wakifanya mji kuwa safi pamoja kuweka salama kwa wananchi kwakuwa sekta binafsi hizo zilikuwa maeneo ya wananchi kiusalama ilikuwa ni Hatari kutokana na Shughulizilizokuwa zikiendeshwa mitaani.
Wajasiriamali hao wamesema eneo ilo walipewa kialali na serikali ili wawezefanya kazi zao kiusalama zaidi kuwa kando na maeneo wanayohishi jamii,walitolewa maeneo mbalimbali wote walipelekwa hapo Tegeta Magereji ili waendelee na shughuli zao za ufanisi wa maendeleo ya kujenga taifa.
Wajasiriamali hao wamedai kuwa leo anajitokeza mwekezaji mgeni na kudai kuwa eneo ilo ni maliyake wakati muda mrefu wako hapo wakikafanya shughulizao za uzalishaji mali,wakiongea kwa masikitiko wamesema hiyo ndiyo ajira yao wakiishi kwa kutegemea shughuli hizo wakiwa na familia zao wanasomesha ,marazi, Chakula pamoja na maitaji yoto ya kibinadamu wakitegemea hapo leo wanaondolewa kama wakimbizi wakati ni wazawa wa Tanzania wataishi vipi
Wamesema eneo ilo awakuvamia wamewekwa kialali na uongozi wa Serikali mwaka 2006 leo wanafukuzwa wataishije na familia zao,NA ikiwa wamekopa na wanadiwa fedha hizo warejeshe Bank.Wamedai itumike ustarabu wa Kuondolewa hapo kwa kufata sheria na haki ya kila mmoja hata hivyo hivi sasa wamekatiwa Umeme pia wameambiwa watabomolewa ,wamedai hikitumika njia hiyo itakuwa si jambo la Busara inaweza kutumia nguvu za ziada zitakoleta mtafaruku wa fujo zitakao rudisha nyuma maendeleo ya taifa.
Wajasiriamali hao wameelekeza kilio chao kwa Mbunge wa eneo ilo Halima Mdee Kiserikali bila kuzingatia maswala ya Itikadi ya Vyama.wajasiriamali hao wameomba wawakilishe kiliochao kwa Serikali pia wamemalinzia kuwa Kesi ya eneo ilo limepelekwa kwenye vyombo vya sheria na kumtaka huyo Mwekezaji afate sheria iliyowekwa na taifa wasinyanyaswe.
Mbunge wa jimbo la Kawe Halima Mdee amewataka wawe na subila kila mmoja hatapata haki yake inayostaili kwa kufuta talatibu zilizopo awawezi kuondolewa kienyeji kwa kuwa walitengewa eneo ilo na serikali kwa kuhamishwa toka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam toka mwka 2006 muda wote huyo mwekezaji alikuwa wapi.
Mhe Halima Mdee amedai atashirikiana pamoja mbaka kieleweke watahakikishwa wanapatiwa eneo lingine pamoja na gharama zote za kuondolewa hapo zitolewe kwa wajasiriamali hao.
Magari yanayotengenezwa na Mafundi hao Tegeta Magereji
Mh:Halima Mdee(Mbunge wa Jimbo la kawe) akiteta na Viongozi wa Tegeta Magereji
Mh:Halima Mdee(Mbunge wa Jimbo la kawe)
Mh:Halima Mdee(Mbunge wa Jimbo la kawe) akiwa na Baadhi ya Viongozi wa Tegeta Magereji
Magari yanayotengenezwa na Mafundi hao Tegeta Magereji
Wafanya Biashara wa Tegeta Magereji wakiwa makini kumsikiliza Mb:Halima Mdee
Mabango yakionyesha kilio cha Mafundi Gereji
MWAKILISHI WA WANAWAKE tegeta magereji.
BRATION MBELWA(Katibu msaidizi wa Magereji)
0 comments:
Chapisha Maoni