Rais
Jakaya Mrisho Kikwete katikati akifurahia kikundi cha Ngoma cha mkoa wa
Ruvuma katika sherehe ya uzinduzi wa Daraja la Ruhekei lililopo katika
barabara Mbinga –Mbamba bay mkoani Ruvuma.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete katikati akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt.John
Magufuli wa kwanza kulia wakifanya ishara ya kuweka jiwe la msingi na
kufungua Daraja la Ruhekei linalounganisha kati ya Mbinga na Mbamba Bay
mkoani Ruvuma.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria kufungua Daraja la Ruhekei
lililopo katika Barabara ya Mbinga-Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe
Magufuli, Mama Salma Kikwete pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali
wakipita juu ya Daraja la Mto Ruhekei baada ya kulifungua mkoani Ruvuma.
Daraja hilo ni kiungo muhimu kati ya Wilaya mpya ya Nyasa pamoja na
Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) kushoto akizungumza na
Mwenyekiti wa kamati ya Miundombinu Profesa Juma Athumani Kapuya (Mb)
kabla ya uzinduzi wa Daraja la Ruhekei lililopo katika Barabara ya
Mbinga-Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) katikati akizungumza na Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe wakati
wakisubiri kuwasili kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa
Dkt.Jakaya Kikwete.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli
wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali mara
baada ya ufunguzi wa Daraja la Mto Ruhekei mkoani Ruvuma.
0 comments:
Chapisha Maoni