Anneth
Peter (katikati) akiwa mwenye huzuni kubwa kutokana na Mshiriki mwenza
kutoka kanda ya Kaskazini Kareb John (hayupo pichani) kutoka kwenye
shindano mara baada ya kuchomwa na jua la utosi.
Kareb John na Malima Deogratius mara baada ya kutangaziwa kuyaaga mashindano..
Mara baada ya Kareb John Kuaga mashindano Mshiriki kutoka kanda ya Kaskazini Annet Peter alionekana mwenye huzuni kubwa
Washiriki wakiwa na huzuni kutokana na wenzao kuaga mashindano.Picha zote na Josephat Lukaza wa Proin Promotions, Dar Es Salaam
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam.
Ni
wiki ya Pili sasa ya mchujo katika Shindano la Tanzania Movie Talents
(TMT) ambapo washiriki wengine wawili wamechomwa na Jua la Utosi na
hatimaye kuaga shindano. Mchujo huo ni muendelezo wa Mchujo ambao kila
wiki washiriki wawili watachomwa na jua la utosi na hatimaye kupelekea
kuaga shindano la TMT.
Mpaka sasa Washiriki wanne tayari wameshayaaga mashindano na kupelekea washiriki 16 kubakia katika mchujo unaofuata.
Mpaka
sasa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limekua ni shindano
lililoteka hisia za watanzania wengi waliopo ndani na nje ya Nchi
kutokana na ubora, Uhalisia na Ubunifu wa hali juu kutoka kwa Waandaaji
na waendeshaji pamoja na washiriki kuonyesha Vipaji vyao.
Ili
kuweza kumnusuru mshiriki wako asichomwe na Jua la Utosi unachotakiwa ni
kumpigia kura kadri uwezavyo ili kumfanya abaki ndani ya Nyumba ya TMT.
Mara
baada ya washiriki wa wiki hii kuondolewa katika shindano hali imezidi
kuwa ni simanzi kwa washiriki kutokana na kutokujua ni zamu ya nani
kutoka wiki ijayo.
Washiriki waliotoka wiki hii ni Kareb John ambae alikua mmoja kati ya Washindi watatu kutoka kanda ya Kaskazini Mkoani Arusha huku Mshiriki Malima Deogratius akiwa ni Mshindi kutoka KAnda ya Pwani Mkoani Dar Es Salaam.
Ili kuweza kumnusuru mshiriki umpendae unachotakiwa kufanya ni Kuandika neno "TMT" ikifuatiwa na namba ya Mshiriki halafu unatuma kwenda namba 15678. Mfano TMT00 tuma kwenda 15678. Piga kura kadri uwezavyo ili kumnusuru mshiriki wako kutochomwa na Jua na Utosi wiki ijayo.
Shindano
la Tanzania Movie Talents (TMT) ni shindano lililobuniwa na Kampuni ya
Proin Promotions Limited ambayo inahusika na utengenezaji, Usambazaji na
Uuzaji wa filamu za Kitanzania huku ikiwa na malengo pia ya Kuibua
vipaji vya Kuigiza na Mpira wa Miguu kwa Wanawake. Shindano hili Pia
linaendeshwa na Kusimamiwa pia na Kampuni bora ya Usambazaji wa Filamu
nchini ya Proin Promotions Limited
Huzuni
na Simanzi zaendelea kutawala ndani ya Nyumba ya TMT kwa washiriki hao
wawili kuondoka lakini Pia Hofu Yaendelea Kutanda ndani ya Nyumba ya TMT
kwa washiriki kwa kutokujua ni zamu ya nani sasa kuchomwa na jua la
utosi litakalompelekea kuaga shindano kwa wiki ijayo.
0 comments:
Chapisha Maoni