SHULE ZA JUMUIYA YA WAZAZI CCM ZAANZA VYEMA KUINUKA KITAALUMA

Jumuiya ya wazazi wa CCM,Tanzania imeitaka jamii kuendelea kuziamini shule zilizopo chini ya jumuiya hiyo kutokana na kuboreshwa na kufanikisha ukuzaji wa taaluma.Hayo yameonekana kwenye matokeo ya kidato cha sita baada ya kufaulisha wanafunzi karibu wote.Wanafunzi waliofanya mtihani huo ni1152 na waliofaulu ni 1143 hiyo kuonyesha ni asilimia ndogo tu walioshindwa kufikia kiwango cha ufaulu.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi amezungumza na waandishi na kuwaasa jamii kuachana na dhana ya kuwa shule hizo zimepoteza muelekeo wakufanya vizuri.Aidha amesema shule zilizotaifishwa kinyemela za jumuiya ya wazazi zimerudi mikononi mwa jumuiya huku akiitaja shule ya kaole moja ya shule zilizorejeshwa katika jumuiya hiyo.

Naye katibu mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ndugu Seif Shabani amesema jitihada kubwa zinaendelea kuhakikisha kuwa zile zilizofanya vibaya zinaboreka zaidi.

Mwisho wamesema umoja wa wazazi Tanzania una shule 70 nchini kote na Miongoni mwa shule hizo 15 ni za kidato cha 5 na 6.


Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Taifa:Ndugu Alhaji Abdallah Majura Bulembo(MCC) na katibu wa Jumuiya ya wazazi Taifa Seif Shabani..

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Taifa:Ndugu Alhaji Abdallah Majura Bulembo(MCC) na katibu wa Jumuiya ya wazazi Taifa Seif Shabani..

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Taifa:Ndugu Alhaji Abdallah Majura Bulembo(MCC) 

Shule ya jumuiya ya wazazi Tanga.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List