Jaji
Vyonne Cherry au Monalisa akitoa maoni kwa washiriki waliokuwa
wameshiriki kwenye filamu fupi iliyochezwa na washiriki wa TMT
Kundi la Kwanza la Washiriki wa TMT waliocheza filamu fupi iitwayo
LUGHA GONGANA wakiwa mbele ya meza ya Pilato katika ukumbi wa makumbusho
ya Taifa mwanzoni mwa wiki.
Mshiriki
wa TMT, Mwanaafa Mwinzago akifunika uso wake kwa kutoamini kuwa
ameponea kwenye tundu la sindano kutokana na kuondolewa katika maumivu
ya Jua la Utosi na kuendelea na mashindano hayo
Mshiriki
Wa TMT, Moses Obunde (Mwenye Suti) akimpongeza Mshiriki Mwenzie Mzee
Kapalata Mtawa kwa kuweza kuondolewa Kwenye Jua la Utosi na Kupelekwa
Kivulini katika Shindano la TMT linaloendelea.
Washiriki
walioingia kwenye Jua la Utosi wakiwa mbele ya Meza ya Pilato huku
mshiriki mmoja kutoka kwa washiriki hao aliyaaga mashindano ya TMT.
Simanzi Zikianzia hapo sasa mara baada ya Washiriki kupunguzwa ili apatikane mmoja wa kuondoka
Wakabaki wawili na hatimaye mmoja kati ya hao aliweza kuondolewa katika mashindano hayo
Baadhi
ya Washiriki wa TMT wakimuaga Mshiriki mwenzao Pendo Edward (Katikati)
ambaye aliweza kutolewa kwenye mashindano kutokana na kura kuwa
chache.Picha Zote na Josephat Lukaza
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam.
Hatua
ya mchujo katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limeingia
wiki ya tatu ya mchujo sasa mara baada ya mshiriki mmoja kuaga shindano
hilo wiki hii. Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limekuwa
shindano bora ambalo kadri siku zinavyozidi kwenda linazidi kuteka nyoyo
za watanzania wengi waliopo ndani na nje ya Nchi kutokana na utofauti
wake na uzuri wake pia.
Mshiriki
mmoja ambaye ni Pendo Edward aliweza kuchomwa na jua la utosi
lililompelekea kutoka kwenye shindano hilo kubwa la Tanzania Movie
Talents (TMT) ambapo mpaka sasa washiriki kumi na tano (15) ndio
wamebaki katika nyumba ya TMT na hali ya simanzi bado inaendelea katika
nyumba ya TMT kwa wiki hii ambapo mshiriki mwingine atatakiwa kutoka.
Shindao
la TMT limekuwa likivuta hisia za watanzania wengi waliopo ndani na Nje
ya Tanzania kutokana na Utofauti wake na ubora wake na kupelekea
watanzania wengi sana kufuatilia shindano hilo kwa ukaribu na umakini
zaidi.
Hatimaye
wiki hii Tanzania Movie Talents iliamua kuzindua Zoezi la kuwapigia
kura washiriki wake kupitia ukurasa wetu wa facebook ambapo sasa
watanzania na wapenzi wa TMT ambao wanauwezo wa kupata na kutumia
internet sasa wanaweza kuwapigia kura washiriki waliowavutia kupitia
ukurasa wetu wa facebook na vilevile kuendelea kuwapigia kura washiriki
kwa kutumia simu zao za mkononi.
Jinsi ya Kumpigia kura Mshiriki umpendae kwa Kutumia Simu ya Mkononi Andika Neno "TMT" ikifuatiwa na namba ya ushiriki halafu tuma kwenda 15678. Mfano TMT 00 tuma kwenda 15678
Na Jinsi ya Kumpigia kura mshiriki kupitia ukurasa wetu wa facebook BOFYA HAPA kwa kupata maelezo.
0 comments:
Chapisha Maoni