WANANCHI KIVULE WALIA NA MRADI WA MAJI MBELE YA NAIBU WAZIRI WA MAJI
-Wananch wa Kivule wakifuatilia maelezo ya Naibu waziri wa maji
Naibu waziri wa Maji Mh AMOS MAKALA
Wanachi wa Mtaa Kipunguni B Kata Kivule jimbo la Ukongo walitoa kelo zao mbele ya Naibu waziri wa Maji Mhe Amosi Makala kuwa Kati zilizopo za utendaji wa Maji sio wahaminifu kwa kuwa wamekuwa wakidanganywa kuhusiana na visima vilivyojengwa na Serikali kwa lengo la kuwanufaisha wananchi ili waweze pata maji salama na safi kwa matumizi ya nyumbani.
Mradi huo wa Visima Kivule ulikuwa ukisimamiwa na shirika la Dawasko ambapo walikuwa wakishirikisha uongozi wa Mtaa bila jamii inayozuguka mradi huo ambapo walikosa uwelewa wa kutambua mradi huo hupo kwa niaba ya wanachi kwa kuwa viongozi wa mtaa huo awakuwa wahaminifu kwa kupotosha jamii na kudai mradi huo ni wa mtu binafsa ambapo sio kweli.
Mwenyekiti wa mtaa wa Kipunguni Bwana Mtoro Muhodeh amekili ni kweli ambapo hata yeye alipotaka kujua Mradi huo wa Visima ni mali ya nani kwa Mtendaji wa Mtaa bi Wilhelmina Ng'ombe na bwana Yasini Kasimu Ngung'unde katibu wa kamati mradi wa maji Kipunguni walitoa maelezo kuwa mradi huo wa mtu binafsi na sio wa wananchi, hali hiyo imebainika kuwa kamati ya maji sio wahaminifu.
Bwana Mtoro ameongeza kuwa tatizo kubwa ni kukosa mawasiliano kati ya Dawasco na wananchi ameongeza akiwataka Dawasco pindi wanapokuwa na mradi wa wananchi waitishe mkutano na kushirikiana pamoja na jamii wasiishie kwenye ngazi za uongozi kwa kuwa watendaji wasio wahaminifu wanahujumu miradi hiyo ya kuwanufaisha wananchi kimaendeleo.
Naye Mnyekiti wa bodi Dawasco Hawa Snalei baada ya kupata taarifa hizo amebaini kutokuwa na mawasiliano mazuri na wananchi pia amesema watalifanyia kazi kwa miradi inayoendelea kutoa taarifa za miradi kwa kujumuisha viongozi pamoja na wanachi husika na mradi,Alimalizia kwa kuwahakikishia wananchi hao mradi huo sio wa mtu binafsi bali ni mali ya wananchi wote hivyo wahitishe mkutano wa kujipanga vizuri waweze kutunza kwa talatibu wa takazo kubaliana ili wanufaike nao.
Naibu waziri wa maji aliwapongeza wananchi hao kwa kutoa kelo yao na imeweza kupatiwa ufumbuzi hata hivyo amesikitishwa na uongozi uliokuwepo kwa kuonyesha tabia isiyokuwa ya uwaminifu kwa wananchi ameweza kukemea jambo ilo na kuwaeleza wananchi wanauwezo wa kufanya mkutano na kuchagua viongozi watakao simamia mradi huo vizuri ili uweze kuleta tija ya maendeleo ya taifa.
Mradi huo wa Kisima utapunguza tatizo la kutembea kwa muda mrefu wa kutafuta maji pamoja na kuvunjika ndoa za wananchi kwa kukosa amani baada ya mama kwenda kutafuta maji kwa kutumia muda mrefu,pia mangonjwa ya Ngozi Kichocho,Tumbo na mengine ya mlipuko yatakuwa yamepatiwa ufumbuzi.
Vikundi vya Sanaa wakijianda kutoa burudani
Mradi wa maji uliotaka kuhujumiwa na viongozi
Mwenyekiti wa Bodi ya maji DAWASCO kulia
Mradi wa maji uliotaka kuhujumiwa na viongozi
Naibu waziri akikabidhiwa zawadi ya mbuzi
0 comments:
Chapisha Maoni