ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MAJI AMOSI MAKALA MAENEO YA GOBA JIJINI DAR ES SALAAM YAINGIA DOSARI



Askali wakiwa makini kusimamia ulinzi baada ya kutokea fujo.

Ziara ya Naibu waziri wa Maji Mh.AMOSI MAKALA maeneo ya Goba jijini Dar es Salaam imeingiwa dosari baada ya kutokea vurugu kati ya wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(chadema) na chama cha mapinduzi(ccm) baada ya kulishiana vijembe na kejeli.

Mh.AMOS MAKALA naibu Waziri wa Maji.

Katika ziara hiyo Mh.AMOS MAKALA amefanikiwa kukamata watuhumiwa watano wakimiliki matenki yenye ujazo wa lita elfu tisa kila mmoja wakitumia maji bila kibali akiwemo mchezaji wa timu ya soka ya Simba wa zamani Dua Said.

Baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa na matenki na matumizi ya maji kulia ni mchezaji wa zamani wa simba Dua Said.


Mh.HALIMA MDEE mbunge wa kawe pia alizungumzia suala la maji ndio tatizo na si siasa hivyo ni muhimu kutatua suala hilo mapema katika jimbo lake.

Mh.HALIMA MDEE mbunge wa kawe

Pia mbunge wa Ubongo Mh.JOHN MNYIKA amekemea kitendo cha wizi wa maji na kuitaka serikali isishie kwa wananchi bali kwa mamlaka husika kwani wamekuwa na mtandao mkubwa.


mbunge wa Ubongo Mh.JOHN MNYIKA

Ziara hiyo inatarajiwa kukamilika alhamisi hii kwa kulitembelea jimbo la ukonga jijini Dar es Salaam.


hali ya fujo ikiendelea kati ya Wanachama wa Chadema na CCM



 Wanachama wa Chadema na CCM wakia katika kurushiana maneno  na kufanya fujo katika ziara.
 Askali wakiwa makini kusimamia ulinzi baada ya kutokea fujo.


polisi wakiwaingiza baadhi ya watu walioleta fujo ndani ya Gari lao la polisi



Mh.AMOS MAKALA akiwa viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa na Mbunge wa Ubongo Mh.John Mnyika.

 Baadhi ya vifaa vya kuhefadhia maji vilivyokamatwa na Mh.AMOS MAKALA
Baadhi ya vifaa vya kuhefadhia maji vilivyokamatwa na Mh.AMOS MAKALA
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List