Hivyo akawataka wasanii kubadilika na kupendana, kushirikiana na kusaidiana bila kujali uzoefu, umaarufu au uwezo wa kiuchumi walionao kwa vile wote wanasafiri katika 'jahazi' moja.
Akizungumza na MICHARAZO, Isike alisema gurudumu la fani ya sanaa hasa ya uigizaji imekuwa ikishindwa kusonga mbele kutokana na wasanii kutopendana na kuoneana kijicho pale mwenzao anapofanya vyema.
Isike alisema hivyo ni wajibu wasanii kubadilika kwani umoja, mshikamano na upendo itasaidia kuwafanya wawe kitu kimoja na kusaidia kupambana na watu wanaowanyonya na kuwaibia kazi zao wanazozitolea jasho kuziandaa.
"Bila umoja, upendo na ushirikiano ni vigumu fani yetu kusonga mbele, wasanii tumekuwa hatupendani wenyewe kwa wenyewe na watu wanaoneana wivu wa kijinga ambao unazorotesha maendeleo ya fani hiyo kwa ujumla," alisema.
Mkali huyo anayejiandaa kutoa filamu yake mpya iitwayo 'Naiogopa Kesho' kupitia kampuni binafsi ya Classic Vision alisema pia wasanii wazoefu wasiogope kuwapiga tafu chipukizi kwa hofu ya kufunikwa kwani hata wao waklisaidia na kupewa nafasi ndiyo maana wapo hapo walipo.
0 comments:
Chapisha Maoni