Mkuu
wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali akiwakaribisha wadau wa
maendeleo ofisini kwake Loliondo walioongozwa na Afisa Miradi ya
Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa tatu
kushoto) aliyefuatana na Meneja Mauzo wa Kampuni a Samsung tawi la
Tanzania , Bw. Slyvester Nteere (wa pili kushoto) pamoja na mwakilishi
wa Ubalozi wa Uswiss nchini, Bw. Eric Kalunga (kushoto) wakiwa na
mwenyeji wao Diwani wa kata ya Ololosokwani, Yannick Ndoinyo (kushoto
kwa DC).
Na Mwandishi wetu, Ngorongoro
Serikali
na halmashauri wilayani Ngorongoro zimetakiwa kutoa ushirikiano kwa
redio za kijamii wilayani humo kwa lengo la kuwaletea maendeleo ya
haraka wananchi wao.
Hayo
yameelezwa na Meneja wa redio ya kijamii ya Loliondo FM, Joseph Munga,
wakati wa ziara ya kukagua miradi inayoendeshwa na Shirika la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) redio hiyo ikiwa miongoni mwa miradi
inayofadhiliwa na UNESCO wilayani hapa wakiambatana na wadau wa
maendeleo kutoka kampuni ya Samsung na Ubalozi wa Uswiss hapa nchini.
‘Redio
za Jamii ndio chombo pekee kinachoziunganisha serikali na jamii katika
suala zima la kujiletea maendeleo’ alisema Joseph Munga.
Mkuu
wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali akiwa kwenye mazungumzo na
wadau wa maendeleo waliofika wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo
inayofadhiliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Munga
aliongeza kwa kusema kuwa redio hiyo iliyoanza kurusha matangazo mwezi
Oktoba 2013 imekuwa ni kichocheo cha kutoa taarifa mbali mbali kwa jamii
wilayani Loliondo na kuibua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii
huku akiitaka serikali na halmashauri wilayani humo kuisaidia katika
kufikia malengo ya kuitumikia jamii na kuwashukuru wadau mbali mbali
wanaoiwezesha redio hiyo ikiwemo kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
ambayo imetoa mnara wao kurushia Matangazo ya redio Loliondo.
“Suala
hapa ni ushirikiano hasa kwa halmashauri kuelewa na kuona umuhimu wa
kutumia redio hii katika matukio mbali mbali yanayofanyika kwenye
halmshauri vikiwemo vikao vya baraza la madiwani ili wananchi
walioshindwa kufika waweze kujua baraza lao limepitisha nini sanjari na
huduma kwenye sekta za afya na elimu”, alisema Munga.
Redio
Loliondo ni miongoni mwa miradi inayofadhiliwa na UNESCO wilayani humo
kupitia asasi isiyokuwa ya kiserikali ya RAMAT kwa kufadhili miradi ya
Maktaba,kutoa elimu kwa jamii ya kifugaji yenye malengo ya kuinua uelewa
na ufahamu kwa jamii hizo zilizopo pembezoni hasa katika suala zima la
kujiletea maendeleo.
0 comments:
Chapisha Maoni