Kutokana na hali hiyo Serikali imeamua kuchimba bwawa kubwa litakalo tumika kuhifadhi maji yatakayotumika kijiji cha Chole na Kwale ila jumla vijiji 28 Vyote vitakuwa vimepata ufumbuzi wa changamoto ya maji kutokana na miradi iliyoandaliwa na Serikali.
Naibu Waziri wa Maji Mh.Amos Makala amesema wakandarasi wote watakaoshindwa kukabidhi mradi kwa wakati au kuhujumu mradi kwa ujenzi usio na kiwango watachukuliwa hatua za kisheria bila kuangalia ni nani au hata kufunga vibali vya kazi.
Mbunge wa jimbo la kisarawe Mh.Seleman Jaffu amewataka wanaanchi wawe na subira ya kusubiri utekelezaji wa miradi kwa kuwa mda si mrefu itatekelezeka na kutatua shida kubwa ya maji.
Uchimbaji wa bwawa kubwa ukiendelea Kisarawe
Naibu waziri wa maji Mh.Amos Makala na Mbunge wa Kisalawe Mh.Seleman Jaffu wakiwa na wataalamu wa maji wakipata maelezo ya ujenzi wa bwawa hilo.
Uchimbaji wa bwawa kubwa ukiendelea Kisarawe
Naibu waziri wa maji Mh.Amos Makala akimtwisha mwananchi maji wakati wa uzinduzi wa maji
Naibu waziri wa maji Mh.Amos Makala akizindua mradi wa maji ya kisima kirefu
Naibu waziri wa maji Mh.Amos Makala
Mbunge wa Kisalawe Mh.Seleman Jaffu
0 comments:
Chapisha Maoni