Diwani
wa kata ya Ololosokwani na Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT)
Bw. Yannick Ikayo Ndoinyo akiangalia kitanda cha kujifungulia wakimama
kwenye Zahanati ya Sero ambayo kwa siku inatibu wagonjwa 50 na zaidi
ikiwa na daktari mmoja huku wakazi wanaofuata huduma hiyo kutoka kata
hiyo na ya jirani Soitosambu kutembea umbali mrefu kwa Kilometa 7-15
kupata huduma ya afya.(Picha Zainul Mzige wa MOblog)
Na Mwandishi wetu, Ngorongoro
Wakazi
wa vijiji vya Ololosokwan, Soit-Sambu, Njoroi na Loipir kata za
Ololosokwana na Soit-Sambu wilayani Ngorongoro wanakabiliwa na
changamoto kubwa ya huduma ya Afya kwa kutembea umbali mrefu kufuata
huduma hizo kwenye kijiji cha Sero huku waathirika wakubwa ni kinamama
na watoto.
Umbali
wa zahanati hizo imekuwa sababu kubwa ya vifo hususani kwa akina mama
wajawazito wanaotaka kwenda kujifungua na watoto halikadhalika
wanapozidiwa hufia njiani kutokana na umbali wa zahanati kutoka kijiji
kimoja kwenda kingine wanapotakiwa kuwahishwa hospitalini hali
inayowafanya kutembea umbali mrefu kilometa 15 hadi kuipata huduma ya
zahanati .
Akizungumza
na waandishi wa habari Diwani wa kata ya Ololosokwani na Mkurugenzi wa
Irkiramat Foundation (RAMAT) Yannick Ikayo Ndoinyo waliotembelea miradi
inayofadhiliwa na Shirika la Elimu na Sayansi (UNESCO) wilayani humo
alisema serikali haina budi kutimiza ahadi yake ya kujenga Zahanati kwa
kila kata nchini Tanzania kuwapunguzia wagonjwa hususan akina mama waja
wazito na watoto adha ya kutembea au kusafiri mwendo mrefu kutafuta
huduma za afya.
Ndoinyo
alisema kuwa tatizo kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma ya afya lipo
na kwamba vifo ya wamama na watoto na kutopata huduma zinazotakiwa kwa
wakati. Wananchi hupata huduma za afya kutoka Sero ambayo ina umbali
mrefu kutoka Ololosokwang au wakati mwingine mgonjwa hupata rufaa rufaa
hadi Hospitali ya wilaya ya Waso na iwapo mgonjwa atakuwa katika hali
mbaya ni tatizo.
Gari
la wagonjwa lilitolewa na serikali likiwa limeharibika kutoka na miundo
mbinu ya barabara na kushindwa kufanyiwa matengezo kwa muda mrefu hali
inayomfanya daktari wa Zahanati hiyo kuwafuata majumbani wagonjwa
mahututi kwenda kuwapatia huduma za afya.
“Utakuta
wagonjwa inabidi watembee umbali mrefu kwenda kupata huduma za afya
kwenye zahanati ya Sero hili ni tatizo tunaiomba serikali yetu
kuliangalia ili kuokoa vifo vya mama na mtoto”alisema diwani.
Ndoinyo
alisema kuwa pamoja na daktari kuwatembelea akina mama na watoto ili
kutoa huduma za afya majumbani kwao kumekuwa na changamoto mbalimbali
hususan vifaa vya vipimo vya kupima magonjwa mbalimbali.
Nae
Mkunga wa jadi Mama Naani alisema mtihani mkubwa unakuja pale wakati
mama mjamzito anapotaka kujifungua na anahitaji huduma ya ziada, hakuna
vifaa na kumlazimu mgonjwa au mama mjamzito kuembea umbali mrefu kupata
huduma hiyo hospitalini.
Madhumuni
ya ziara hiyo inayowashirikisha wawakilishi kutoka Kampuni ya Samsung
na mwakilishi kutoka ubalozi wa Uswiss hapa nchini ni kujionea miradi
mbalimbali inayoendeshwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) inayotekelezwa na redio ya Jamii Loliondo wilayani Ngorongoro.
Miongoni
mwa miradi inayofadhiliwa wilayani humo ni pamoja na Redio Loliondo
ambayo pia inafadhiliwa na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel kwa
kurusha matangazo yake kupitia mnara wa kampuni hiyo na Mradi wa Maktaba
unaolenga kuwapatia wanafunzi uelewa wa mambo mbalimbali yanayohusu
masomo ya sayansi.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph,
akishanga kitanda cha kujifungulia wakinamama kwenye zahanati hiyo
ambayo ina uhaba wa vifaa mbalimbali vya matibabu huku halmashauri
ikishindwa kumalizia majengo ya wodi kwa ajili ya kulaza wagonjwa ambapo
imeonyesha wakina mama na watoto wamekuwa wakifia njiani kutokana na
kutembelea umbali mrefu kufuata matibabu.
Vifaa
vinavyotumika kwenye zahanati hiyo wakati wakinamama wanapojifungua,
jingine ni Friji kwa ajili ya kuhifadhia chanjo mbalimbali za watoto na
kinamama linalotumia umeme wa jua.
Daktari
wa Zahanati ya Sero kata ya Ololosokwani Dkt. Veronika Nyoni (katikati)
akielezea changamoto mbalimbali anazokumbana nazo katika kutoa huduma
ikiwemo Umeme na kupelekea kutumia tochi wakati wakinamama
wanapojifungua ambapo ameiomba serikali kupitia wafadhili mbalimbali
kuwasogezea hata huduma ya umeme jua ili kukabiliana na changamoto
hizo.Kulia ni Mwanahabari wa gazeti la Zanzibar leo, Mahmoud Ahmad na
kushoto ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw.
Al Amin Yusuph wakimsilikiliza kwa makini Dkt. Nyoni.
Diwani
wa kata ya Ololosokwani na mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT)
Bw. Yannick Ikayo Ndoinyo akiwa na wadau wa maendelo wakiongozwa na
UNESCO waliofanya ziara katika kata ya Ololosokwani wilayani
Ngorongoro. Katikati ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa
UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph na kulia ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya
Samsung tawi la Tanzania, Bw. Slyvester Nteere.
Nyumba
ya Daktari Mstaafu aliyekuwa akitoa huduma katika zahanati ya Sero
zaidi ya miaka 25 kama inavyoonekana ikiwa na Umeme wa jua pamoja na
Dish ikiwa ni maendeleo katika eneo hilo lililopo karibu na pori tengefu
la Loliondo.
0 comments:
Chapisha Maoni