WAGOSI WA KAYA WAISHIKISHA ADABU POLISI MORO, WAITANDIKA 2-0 'COASTAL DAY' MKWAKWANI



TAMASHA la ‘Coastal Day’ limefanyika leo katika uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga ambapo mashabiki na wanachama wa klabu hiyo wamepata nafasi ya kuwaona wachezaji wapya waliosajiliwa majira ya kiangazi mwaka huu.
Coastal walioweka kambi ya mwezi mmoja kisiwani Pemba wamecheza mechi ya kirafiki na Polisi Morogoro ili kusindikiza tamasha hilo.
Afisa habari wa Coastal Union, Oscar Assenga amesema wagosi wa kaya wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu hiyo mpya ya ligi kuu msimu ujao.
Assenga alisema mabao ya Coastal Union yalifungwa katika dakika ya 35 na Ramadhan Salum aliyesajiliwa kutokea Gor Mahia ya Kenya na la pili likafungwa na Iker Bright Obina.
Baada ya mechi hiyo wachezaji wapya walitambulishwa mbele ya mkuu wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego akiambatana na mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Ahmed Aurora.

Picha za matukio ya tamasha hilo zitakujia muda wowote.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List