JUMUIYA YA WAZAZI CCM YAPATIWA PIKIPIKI 170 KWA MAKATIBU WA WILAYA TANZANIA.
-Chama cha mapinduzi kwa Kupitia Jumuiya ya Wazazi imetoa pikipiki 170 kwa makatibu wote wa wilaya kwa lengo la kuimarisha chama na kujiandaa na uchaguzi mkuu.
Lengo la Pikipiki hizo ni kupunguza kero ya Usafiri na kuwafanya makatibu kufikia pande zote za nchi.Ndugu Abdallah Bulembo Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Taifa akikabidhi pikipiki hizo amesema ni kiungo muhimu katika kupashana Habari na kufanya majukumu ya chama kwa Uhakika.
Dr Muhammed Seif Khatibu ni katibu wa organaizesheni Taifa ambaye kwa upande wake ameitaka Jumuiya ya Wazazi kujipanga vizuri kipindi hiki.
0 comments:
Chapisha Maoni