MGOMBEA URAIS ADC

Mbio za kuelekeza kwenye kinyang'anyio cha uchaguzi  mkuu zinazidi  kuendelea  nchini  ambapo  makada  watatu wa chama cha alliance democratic  change-ADC  wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi ya urais kupitia chama hicho



Mfanya biashara  maarufu jijini Dar es Salaam Abubakari Rekesh ambaye ni mlemavu wa viungo ni miongoni mwa  watia nia watatu wakiwamo Chief Lutalopa kutoka kigoma pamoja na Emanue Faustini lutoka Mwanza ambao wamechukua fomu za kuomba kuteuliwa kupeperusha Bendera ya chama hicho kwenye nafasi ya Urais

Abubakari Rekesh endapo wananchi wata mchagua kuwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania amesema atakuwa na maamuzi magumu kwa watu watakao bainika kuwa ni wauwaji kwa watu wenye ulemavu wa ngozi Albino , Vikongwe, hukumu yao itakuwa ni kifo kwa upande wauza dawa za kulevya nchini , walarushwa hukumu yao miaka hamsini jela .  Amemalizia na kusema yeye ni miongoni mwa viongozi waadilifu anaye thamini kila mwananchi, mwenye mikakati ya kuleta maendeleo ya taifa

Mbunge wa Wawi Hamed Rashidi Mohamed akiutubia katika mkutano huo amewataka wananchi wajitokeze kujiandikisha  katika daftari la kudumu la kupiga kura ili watumie hakiyao  ya msingi wakati  wa uchaguzi ukifika kuchagua kiongozi atakaye wafaa, pia ametaka tume ya uchaguzi wasimamie zoezi hili liweze kufanikiwa watende haki kwa vyama vyote vya kisiasa wasiangalie vyama vikubwa tu






Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List