Rais Jakaya Kikwete amesema hakuana mgombea ama mwana siasa anayeweza kuwanunua watanzania wote,ili wamuunge mkono kwenye juhudi zake za kushika wadhifa anaowania huku wakimnadi mgombea wa chama cha mapinduzi.,Dkt John magufuli kuwa ni kiongozi mwenye uwezo na uzowefu mkubwa
Aidha Rais Kikwete amewetaka wana ccm kujitokeza kwa wingi kumpigia kura mgombea wao ili aweze kushinda na kuendeleza yale ambayo tayari serikali ya awamu ya nne ilioanza kuyatekeleza.
Alipokuwa akizungumza na wazee wa ccm wa mkoa wa dar es salaam rais Kikwete amesema wapo baadhi ya wana siasa wanaotanguliza fedha ili kuwanunua watanzania wawaunge mkono kwenye nafasi wanazogombea ambapo amesema hata wakifanya hivyobado hawatofanikiwa kuwanunua watanzania wote.
Mgombea wa Urais kpitia chama hicho Dkt John Pombe Magufuli aliyeambatana na Rais Kikwete yeye kwa upande wake pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kumpa furs hiyo huku akiwaidi kuongoza nchi kwa kuzingatia kwamba Tanzania ni Moja.
Rais kikwete aliongozana pia na Mgombea mweza wa Urais CCM Samia Suluhu,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ramadhani Madabida na viongozi wengine wa Chama na Serikali na Lengo kubwa likiwa ni kuwaomba wazee hao kumuunga mkono mgombea wa sasa Dkt Magufuli katika safari yake.
TAWA YASHEREHEKEA SIKU YA WANYAMAPORI DUNIANI
-
🔴🔴 TAWA Yasherehekea Siku ya Wanyamapori Duniani kwa Kutoa Misaada na
Elimu ya Uhifadhi
Akikabidhi misaada hiyo na miche ya miti Kaimu Kamanda wa Uh...
Saa 8 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni