Chama cha mapinduzi(CCM) mkoa wa dar es salaam kitazindua rasmi kampeni zake za kuelekea katika uchuguzi mkuu unaaotalajia kufanyika october 2015 mwaka huu.Kampeni hizo zitazinduliwa katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam ambapo pia kitamnadi Mgombea wake wa Urais Dr John Pombe Magufuli.
Katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Dar es salaam Juma Simba Gadafi anasema kampeni za chama hicho kwa upande wa Dar es salaam zitaendeshwa kistaarabu na kuwataka baadhi ya wakazi wa jiji hilo kuacha kuwatolea maneno yasiyofaa wafuasi wa chama hicho.
Aidha Juma Gadafi amesema kila mtu anayo haki ya kushabikia chama anachokipenda na kuongeza kuwa udhalilishwaji unaofanya na baadhi ya watu hauna manufaa.
Kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu zimeanza ambapo vyama mbalimbali vya siasa vinajinadi ili viweze kuchaguliwa kwenye uchaguzi mkuu ambapo kwa Mkoa wa Dar es salaam pekee kuna Majimbo 10 na kata 102.
UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO
-
UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO
Saa 6 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni