Jeshi la wananchi wa TANZANIA JWTZ limeeleza mafanikio yake ya miaka 30 ya uzalishaji wa tecknolojia mbalimbali katika kambi ya NYUMBU iliyoko mkoani Pwani.
Kambi hiyo ilianzishwa mwaka 1985 kwa ajili ya kufanya utafiti na kuendeleza uvumbuzi na ubunifu wa teknolojia ili kuongeza uwezo wa Tanzania kujitegemea.Akizungumza na waandishi wa habari katika kambia ya NYUMBU,Mkurugenzi wa shirika la Nyumbu Brigedia Jenerali Anselm Shigongo amesema shirika lao limepewa majukumu sita ikiwemo kufanya usanifu wa magari na mitambo kwa ajili ya kuzalisha nchini.
Akizungumzia maendeleo ya uzalishaji katika shirika Luten Kanali Juma Nkangaa,anasema iwapo shirika hilo litawezeshwa na kupitishwa bajeti iliyotengwa na serikali ya shilingi bilioni sita linaweza kulibeba Taifa katika sekta mbalimbali za maendeleo.
Naio wahandisi wa miradi ya uzalishaji katika teknolojia za ujenzi na vipuri,wamezungungumzia uzalishaji wa teknolojia hizo katika shirika hilo la Nyumbu.
Shirika la Nyumbu lilianzishwa Desemba 14 mwaka 1985 kwa lengo la kuwa kituo maalum, nchini kwa ajili ya kufanya utafiti na kuendeleza uvumbuzi na ubunifu wa teknolojia,
KAMATI YA SIASA YARIDHISHWA NA HUDUMA YA MAJI TUMBI
-
Na Clemence Kagaruki
Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu Chana Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Kibaha
Mjini ikiongozwa na Mwenyekiti Mwl. Mwajuma Nyamka ime...
Saa 1 iliyopita
0 comments:
Chapisha Maoni