Tume ya haki za binadamu imeandaa chumba maalumu kitakokuwa kikipokea taarifa za zoezi la upigaji kura kutoka kila kituo nchini kote,ili kuhakikisha aliyejiandikisha atatumia haki yake ya msingi ya kuchagua kiongozi anayemtaka .
Aidha imesema itahakikisha uchaguzi mkuu unakuwa huru na wa haki kwa kutogubikwa na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu na kuhaidi kusimamia kila hatua ya zoezi hilo.
Kituo cha sheria na haki za binadamu kimesema kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali kimejipanga kuhakikisha watanzania wanapata fursa ya kupiga kura kwa uhuru.
Mtandao wa TASEO utakao shiriki kwenye mchakato huo ,umeeleza kutambua vijana wengi watakao shiriki kwenye uchaguzi mkuu,hivyo kuona haja ya kuwashirikisha kikamirifu kwenye hatua hii ya kulinda kura zao.
ENEO LA HIFADHI YA NGORONGORO NI URITHI WA DUNIA, TUENDELEE KULITUNZA; DKT.
MPANGO.
-
Mwandishi wa NCAA, Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor
Mpango amesema eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ambalo n...
Siku 1 iliyopita
0 comments:
Chapisha Maoni