Wafanya biashara wa soko kuu la kariakoo jijini dar es salaam wameiomba serikali kuruhusu magari ya mizigo kufika katika soko hilo kwani wanaathirika kiuchumi kutokana na kukosekana kwa bidhaa.
Wafanya biashaa hao wamelalamikia Manispaa ya Ilala kwa kupandisha ada ya vibali na masharti ya muda wa kuingia katika soko hilo,Mambo ambayo yamesababisha wakulima kushindwa kufikisha bidhaa zao katika soko hilo,Na baadala yake kupeleka katika masoko mengine.
Meneja wa soko hilo Florens Saiya amesema licha ya changamoto kuwa nyingi katika eneo hilo la soko lakini mapato yamekuwa yakiongezeka na tatizo la kukatika umeme limepatiwa ufumbuzi kwa ununuzi wa jeneleta kubwa la kuzalisha nishati hiyo ya umeme.
Afisa Biashara wa manispaa ya Ilala hakupatikana kuzungumzia lalamiko hilo la wafanya biashara wa soko hilo.
TUMETIMIZA MATAKWA YA ILANI YA CCM YA KUFIKISHA WATALII MILIONI TANO-DKT
CHANA
-
Na Mwandishi wetu, DSM
Waziri wa Maliasili na Utalii mhe. Balozi Dkt.Pindi Chana (Mb)
amewapongeza watendaji wa wizara hiyo kwa kutimiza malengo ya ilan...
Saa 15 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni