Wanawake wamelalamikia ubaguzi katika uteuzi wa wagombea kuwania nafasi mbalimbali za uongozi Tanzania.Wanawake hao wamelalamika katika mkutano wa wanawake kwamba vyama vyote vya siasa vimetoa fursa ndogo kwa wanawake nchini kushiriki katika uchaguzi huo.
Kwa upande wa CCM wanawake mamelalamikia kura za maoni kuwa zilitawaliwa na rushwa na vikao vya maamuzi vilishindwa kuwatetea wanawake walionyesha uwezo mzuri wa kisiasa na uongozi.
Kwa upande wa UKAWA wamelalamikia muungano huo kushindwa kutoa kabisa fursa kwa wanawake kutokana na utaratibu wa kugawanywa majimbo kwa vyama vinvyounda UKAWA,mfumo huo ambao umeonekana ni mbovu na kutoa fursa chache kwa wanawake,Pia wamelalamikia chama cha CUF kwa kushindwa kutoa fursa kwa wanawake .
Wanawake hao wamepaza sauti kwa upande wa Tanzania visiwani kwa kuonyesha mwitikio mdogo kwa wanawake walionyesha nia ya kuwa viongozi na kushauri mshikamano ili kumkomboa Mwanamke wa Tanzania.
UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO
-
UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO
Siku 1 iliyopita
0 comments:
Chapisha Maoni