Jumuiya ya wazazi bagamoyo kupitia mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya bagamoyo Abdul Sharif amesema hivi sasa wamevunja makundi baada ya kupita kura za maoni na kupata mwakilishi wa ccm.
Kwa kupitia jumuiya ya wazazi watahakikisha wanafanya kampeni nyumba kwa nyumba na kuwashawishi wananchi wajitokeze kupiga kura na kumchagua kiongozi atakayeleta maandeleo mwenye uwezo na sifa thabiti Dr.Shukuru Kawambwa.
Kwa kuwa ameonyesha anauwezo wa kutatua matatizo mbalimbali ya uchumi na kijamii pia amesema kwa jumbo la CHALINZE mgombea anayefaa kupeperusha bendera ya ccm ni Mh.Ridhiwani kikwete hayo ameongea akiwa CHALINZE kwa ajili ya maandalizi ya kampeni za ubunge.
Kampeni kwa wilaya ya bagamoyo kwa jumbo la CHALINZE itazinduliwa rasmi 16 mwezi huu na Mgombea mweza wa Ccm kiti cha urais.na Bagamoyo itakuwa tarehe 17.
Akiongea na mwandishi wa blog Dr Shukuru Kawambwa amesema katika ahadi zake amefanikiwa kutimiza asikimia 80 katika utekelezaji wa Irani ya Ccm na kufanikiwa katika masuala ya Elimu,Afya,miundombinu na uvuvi pia ameamua kuchukua fomu ili kukanilisha machache aliyoyaacha na kufanya mabadiriko ya kweli kwa jamii.
Pia amewataka wananchi kumpigia kura na kutoa ushieikiano kwa viongozi wote wa Ccm kuanzia nafasi ya urais mpaka madiwani.
0 comments:
Chapisha Maoni