Umoja wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Taifa wamempongeza Rais Dk John Pombe Magufuli kwa juhudi zake za kuhakikisha huduma za kijamii, zinarejea kwa watu wote nchini Pongezi hizo zimekuja kufuatia maelekezo ya Magufuli kuwa fedha za sherehe za Wabunge zilizochangwa na taasisi mbalimbali zipelekwe kununulia Vifaa Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na maelekezo mengineyo yanayotaka matumizi ya fedha za umma kudhibitiwa Abdallah Bulembo ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa anapongeza jitihada,za Rais Magufuli Katika utendaji kazi wake huku akiwataka Watanzania wote kumuunga mkono
MAGUFULI APONGEZWA KWA UTENDAJI WA KAZI NA JUMUIYA YA WAZAZI CCM TAIFA
-
07:20
0 comments:
Chapisha Maoni