Aliyekuwa waziri mkuu nchini Tanzania na mwanachama wa Chama cha Chadema Edward Lowassa, amehojiwa na kuondoka katika afisi ya mkurugenzi wa uchunguzi wa jinai baada ya kutakiwa kufika katika afisi hiyo siku ya Jumatatu kwa sababu zisizojulikana .
Kulingana na gazeti la The Citizen, Bwana Lowassa ambaye alitakiwa kuwasili katika afisi ya DCIO muda wa saa nne aliwasili saa tatu na dakika 58 asubuhi.
Msafara wake ulikuwa na magari sita ikiwemo magari mawaili ya polisi yaliokuwa na polisi waliojihami.
The Citizen linasema kuwa usalama ulikuwa umeimarishwa katika barabara ya Ohio.
Waandishi habari walikatazwa kuchukua picha za bwana Lowassa.
Katika mahojiano ya simu na gazeti la The Citizen, alisema kuwa anashuku kwamba agizo hilo la kutakiwa kujiwasilisha linatokana na matamshi aliyotoa mjini Dar es salaam siku ya Ijumaa wakati wa hotuba ya Iftar.
Wakati wa hotuba hiyo, alimtaka rais Magufuli kuwaachilia huru wahubiri wa Kiislamu ambao walikuwa wamekamatwa kwa zaidi ya miaka minne bila kesi zao kuamuliwa.
KAMA UNA UGOMVI NA MTU KARIBU MAPOROMOKO YA MAJI ENDORO
-
Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro imeanza utekelezaji wa mpango
maalum wa kuboresha eneo la Endoro ili litumike kama sehemu ya utalii tiba
kwa wa...
Saa 5 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni