Tanzania imekuwa kivutio kikubwa cha watalii kutoka mataifa mbalimbali hususani maeneo ya Serengeti National Park na Mlima Kilimanjaro.
Msanii maarufu wa Marekani Usher Raymond pamoja na familia yake wapo ziarani nchini Tanzania, na leo wametembelea eneo la hifadhi ya wanyama pori la Serengeti National Park.
Raymond kupitia ukarasa wake wa twitter ameweka picha ikionesha yupo katika hifadhi hiyo wakifurahia mazingira yeye na familia yake.
“So amazing to experience this beauty with my family” ameandika Usher Raymond kwenye kurasa wake wa twitter wakati akiwa katika hifadhi ya taifa ya Serengeti.
WAANDISHI WA KIMATAIFA WAKOSHWA NA UZURI WA NGORONGORO
-
Waandishi nguli wa habari za michezo na burudani kutoka sehemu mbalimbali
duniani, walioko nchini Tanzania kwa ziara ya kiutalii na kufuatilia
maandali...
Saa 19 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni