Majaliwa amtumbua DED wa mbozi kwa matumizi mabaya ya fedha za umma
Katika kuhakikisha kunakuwepo na matumizi mazuri ya fedha za umma, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe, Eliseyi Mgoyi pamoja na maofisa wengine watatu kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma.
Majaliwa amewasimamisha kazi maofisa hao mapema hii leo wakati alipozungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Vwawa, akiwa katika ziara yake ya kikazi.
Amesema kuwa Maofisa hao wamekiuka sheria za matengenezo ya magari ya Serikali kwa kwenda kutengeneza katika gereji ambazo hazikusajiliwa na wala hazifanyi shughuli hiyo, jambo ambalo halikubaliki.
“Halmashauri inanuka rushwa tunataka iwe safi. Hatuwezi kukubali kuona Halmashauri hii na zingine nchini zikigeuzwa kuwa magenge. Kwa Serikali hii no, hatuhitaji rushwa wala harufu ya ufisadi.”amesema Majaliwa
Aidha, amesema kuwa Serikali haiwezi kuvumilia kuona watumishi waliopewa dhamana wakijinufaisha kwa fedha za umma na kuwaacha wananchi wakiendelea kuteseka kwa kukosa huduma mbalimbali za kijamii zikiwemo za maji, afya na elimu, hivyo itaendelea kuwachukulia hatua.
Hata hivyo, Majaliwa amewataka Madiwani na Wakuu wa Idara katika Halmashauri zote nchini wabadilike na wahakikisha wanashirikiana na kufanya kazi kwa ushirikiano kwani wakigawanyika watashindwa kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi.
Home / gloria media
/ DED WA MBOZI NA MAOFISA WENGINE WATATU WASIMAMISHWA KAZI KWA TUHUMA ZA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA UMMA.
- Blogger Comment
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Inaendeshwa na Blogger.
About Me
Wanaofuata
TANGAZO
My Blog List
-
-
SUPER D AMUANDAA SUNDAY KIWALE KWA USHINDI WA K,O JANUARY 31 TANGA ATAKAPOZIPIGA NA YOHANA MCHANJA - SUPER D AMUANDAA SUNDAY KIWALE KWA USHINDI WA K,O JANUARY 31 TANGA ATAKAPOZIPIGA NA YOHANA MCHANJA Na Mwandishi Wetu KOCHA wa kimataifa wa mchezo wa masum...Miaka 5 iliyopita
-
SUPER D AMUANDAA SUNDAY KIWALE KWA USHINDI WA K,O JANUARY 31 TANGA ATAKAPOZIPIGA NA YOHANA MCHANJA - Na Mwandishi Wetu KOCHA wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye kwa sasa anamnowa bondia Sunday Kiwale 'Moro Best' kwa aj...Miaka 5 iliyopita
-
BONDIA MAKUBI ATAMBA KUMPIGA ABDALLAH MA MOROGORO OKTOBA 4 KATIKA UKUMBI WA 361 MWENGE - Na Mwandishi wetu Bondia Ibrahim Makubi yupo kambini kwa ajili ya mazoezi yake ya kumkabili bondia abdallah kingolwira wa ( morogoro ) katika pambano l...Miaka 5 iliyopita
-
JUMA CHOKI AJIANDAA NA MASHINDANO YA KING OF THE RING JULAI 28 - Bondia Ibrahimu Makubi kushoto akioneshana umwamba na Juma Choki wakati wa Mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Super D iliyopo shule ya Uhuru Kariakoo...Miaka 5 iliyopita
-
0 comments:
Chapisha Maoni