Makonda kumaliza msongamano katika hospitali Dar es salaam
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amekagua wodi ya akina mama katika Hospitali ya Amana iliyopo Ilala Jijini Dar es salaam.
Katika ukaguzi huo Makonda amesema kuwa kukamilika kwa wodi hiyo kutasaidia kuondoa msongamano mkubwa uliokuwepo kipindi cha nyuma hivyo amewaasa wahusika kutunza wodi hiyo.
Aidha, ameongeza kuwa katika idara ambayo anaamini kuwa itafanya vizuri katika mkoa wa ni sekta ya afya kwa kuwa watu wengi wamekuwa wakijitolea kusaidia katika sekta hiyo. Pia amewashukuru watu wote waliojitolea kuweza kuchangia hivyo amewaasa wananchi kujitokeza kuungana na Serikali katika kuujenga mkoa wa Dar es salaam.
WABUNGE WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUTOA BILIONI 10.4 KUJENGA MAKAO MAKUU
MAPYA YA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO.
-
Na Mwandishi wetu.
Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii
wameipongeza na kuishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongo...
Saa 6 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni