TEMEKE WAHITIMISHA KAMPENI ZA UCHAGUZI KWA KISHINDO.

Jimbo la Temeke wafunga kampeni za uchaguzi katika kata ya Sandari wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam kupitia chama cha Mapinduzi.                                                      

Kampeni hizo zimefungwa na Mjumbe MNC  Richard Kasesela wakati akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Temeke Mariamu Kisangi kupitia chama cha Mapinduzi na mgombea Udiwani Mrisho Kamba kata Sandari. 


           

Akiwa anafunga kampeni Amewaomba Wananchi wachague Ccm kuanzia  ngazi ya Urais Mama Samia Suluhu Hassani,Ubunge Mariamu Kisangi na Udiwani Mrisho Kamba ili wafanye kazi kwa pamoja ya kuleta maendeleo. 

    


Ndugu Mrisho ameomba kura kwa Wananchi wamchague ili atekeleze ilani ya chama cha mapinduzi ikiwa na pamoja kutengeneza barabara zote korofi na kumaliza kabisa usumbufu kwa watumiaji wa njia hiyo.


Pia atahakikisha Kituo cha afya kinajengwa ili wagonjwa wanaoenda kutibiwa Temeke wapate ahueni kutokana na  umbali mrefu uliopo na Masuala yote ya uzazi na watoto yatashughulikiwa na kutatuliwa kabisa.

Akiendelea kujinadi amesema fedha zinazotolewa na Manispaa zisizokuwa na riba asilimia 25 zinawafikia walengwa akina mama asilimia 10 vijana asilimia 10 na Walemavu asilimia 5.Huduma za Elimu na maji zinaboreshwa na kuwafikia wanachi kwa ukaribu kabisa.Hata hivyo amewaomba na kusisitiza wamchague Rais Mama Samia Suluhu na Mbunge Mariamu Kisangi.


 Kampeni hizo zimefungwa na wananchi wametakiwa wajitokeze kupiga kura kumchagua kiongozi wanaye mtaka wasiogipe maneno yanayosemwa.




















MWISHO                                 

Share on Google Plus

About SDM PRODUCTION MEDIA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List