RAIS KIKWETE ATAKUWA MGENI RASMI KATIKA TAMASHA LA WAKULIMA NA WAJASILIAMALI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kufungua tamasha la wakulima na wajasiriamali litakalofanyika katika viwanja vya Chuo cha Sanaa Bagamoyo Septemba 16 hadi Septemba 21.

Meya wa mji mdogo wa Bagamoyo, ambaye pia ni mwenyekiti wa maandalizi ya Tamasha hilo, Abdul Zahor Sharif

Tamasha hilo linatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh 100milioni za kitanzania na limeratibiwa na taasisi ya Twisuka.

Mwenyekiti wa maandalizi ya Tamasha hilo, Abdul Sharif aliiambia blog hii kuwa lengo la tamasha hilo ni kuinua uchumi kwa wakulima na wajasiriamali waliopo wilaya ya Bagamoyo.

Sharif alisema pia baada ya tamasha hilo kutaanzishwa chombo cha kuwasaidia wakulima na wajasiriamali katika wilaya hiyo ili wanufaike kiuchumi na kijamii kwa kupitia fursa mbalimbali zilizowazunguka.

Sharif pia amewaoma wadau mbalimbali toka ndani ya bagamoyo na nje ya mji huo kujitokeza kusaidia kufanikisha tamasha hilo hata hivyo alisema washiriki katika tamsaha hilo watakuwa tisa kutoka kila kata, wilaya hiyo inakata 22.

Naye msemaji wa Tamasha hilo, Groria Matora, alisema lengo linguine la tamasha hilo ni kuwawezesha wajasiriamali na wakulima wa wilaya hiyo kupata masoko, ubunifu, mitaji na elimu ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali kupitia fursa zinazowazunguka katika wialaya hiyo.
 

Meya wa mji mdogo wa Bagamoyo, Abdul Sharif wakipongezana baada ya kukamilisha kamati zitakzosimamia majukumu katika kufanikisha tamasha hilo na Afisa Habari wa Tamasha hilo, Gloria Matola pembeni kulia ni Mkurugenzi wa Twusoka na wengine ni wanahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini.
Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List