KUNDI la
sanaa la ngoma na maigizo, lenye jina la Kijichi Sanaa Group,
kilichopo Kijichi wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam wameiomba
Serikali iwasaidie mtaji ili kufanikisha kurekodi kazi
zao za sanaa.
Kundi
hilo lenye jumla ya vijana 24, linazaidi ya miaka saba na limeshapata
usajili toka Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) Septemba 23, 2011 kwa jina la
Kijichi Sanaa Group, halijawahi kurekodi kutokana na kutokuwa na mtaji wa
kutosha kufanikisha jambo hilo.
Msemaji wa kundi
hilo, Ahmed Mshiraz aliomba serikali kusaidia vijana wanaojituma katika
kazi za sanaa kwa kutumia vipaji walivyonavyo ili kuondoa umaskini
unaowazunguka.
Mshiraz aliongeza
kuwa vijana wengi wamekata tamaa baada ya kukosa uwezeshwaji licha ya
kujituma kwa uwezo wao wote kuonyesha vipaji vyao hali inayochangia vijana
kijihusisha na vitendo viovu vikiwemo uporaji, matumizi ya dawa za
kulevya, ubakaji, ushoga, usagaji na kazi haramu kama ujangiri.
Naye
mwenyekiti wa kundi hilo, Maulid Mbarouk
ameiomba serikali na wadau wa maendeleo kujitokeza kusaidia mitaji, ili
vijana hao waweze kutoa kazi walizonazo ambazo wanashindwa kuzitoa kutokana na
kutokuwa na mtaji wa kuwawezesha kurekodi kazi hizo.
Mbarouk alisema
alisema kundi ilo linajiushughulisha na sanaa za ngoma, filamu, uimbaji,
mpira, mapishi pamoja na maswala ya manzingira ambapo hujitolea kufanya bure
kwenye mitaa mbalimbali nchini.
Pia kundi hilo
linaomba mtu yeyote mwenye uwezo wa kulizamini kundi hilo ajitokeze ili
kuendeleza vipaji vya vijana hao na kuwawezesha kufikia malengo yao ikiwemo
kurekodi kazi zao.
0 comments:
Chapisha Maoni