JUMUIYA ya akina mama wasiojiweza kiuchumi 120 wanaoishi
kata ya Tabata jijini Dar es salam wamepewa mafunzo ya mwezi mmoja ya Ujasiriamali
ili kuwakomboa Kiuchumi.
Mafunzo haya yamejumuisha utengenezaji wa Batiki, Vikoi, utengenezaji
wa mafuta, Sabuni na Usindikaji wa vyakula na matunda.
Akina mama hawa waliopewa mafunzo na Taasisi binafsi ya Tiba
mbadala ya GHCHC wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa mitaji na upatikanaji
wa soko la uhakika la bidhaa zao.
Umoja huo pia umewezeshwa na mtaji wa kianzio wa Sh 100,000
kutoka mfuko wa PSPF ambao unawapa mwanzo mpya.
Mratibu wa mafunzo hayo, Ferdinand Ngowi alisema wameamua
kuunga mkono jitihada za Serikali za kuwakwamua wakinamama kiuchumi.
0 comments:
Chapisha Maoni