Wachezaji wakisalimiana muda mchache kabla ya mtanage kuanza
Wachezaji wa timu ya Kashai wakiomba uwanjani
Wachezaji wa Rwamishenye.
Na Faustine Ruta, Bukoba
Timu ya Rwamishenye imeibuka Shujaa na kufanikiwa kutinga katika hatua ya fainali ya michuano ya KAGASHEKI CUP 2013 baada ya kuchomoza na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Kashai Fc. Rwamishenye ndio walioanza kufunga bao kupitia mshambuliaji Khalid Seleman kipindi cha kwanza nao Kashai wakiongeza bidii na kuweza kusawazisha bao hilo kipindi hicho hicho cha kwanza kupitia mchezaji wao Paulo Manu. Kipindi cha kwanza kikimalizika timu zote zikiwa nguvu sawa.
Kipindi cha pili kilitawaliwa
na timu ya Rwamishenye huku wachezaji wa timu ya Kashai Fc wakizembea kukaba
wenzao na kuchoka wachezaji wa Rwamishenye wametumia nafasi hiyo na kuweza
kuwaongezea bao la pili kupitia mchezaji wao matata Hassan Hussein aliyeingia
kipindi cha pili kwa mkwaju mkali uliompita mlinda mlango wa timu ya Kashai katika dakika ya 75.
Ushindi huu walioupata
Rwamishenye unawawezesha kutinga hatua ya Fainali siku ya Jumamosi hii tarehe
17 Agosti kuwavaa washindi walioifunga timu ya Makhirikhiri (Kitendaguro Fc)
jana ambao ni Bilele FC katika uwanja wa Kaitaba.
Mchezo huu pia umeweza
kuingiliwa na sintofahamu baada ya mashabiki wa timu ya Kashai Fc kuanza
kufanya vurugu na kurusha mawe dakika za mwishoni baada ya kuona timu yao
imefungwa na jambo hilo limeweza kunyamazishwa na askari waliokuwa uwanjani
humo na kuweza kuwaokoa wachezaji na waamuzi wa mtanange huo wasidhurike.
Waamuzi wa mtanange huuKikosi cha timu ya Rwamishenye kilichoanza
Mtanange ukiendelea...punde!!
Hatari kwenye lango la timu ya Rwamishenye..
0 comments:
Chapisha Maoni