MOSCOW, Russia
BINGWA wa masumbwi duniani katika uzani wa WBA, Wladimir Klitschko (pichani), anatarajia kupanda ulingoni kumvaa bondia asiyepigika raia wa Russia, Alexander Povetkin.
Pambano baina ya miamba hiyo ya 'ndonga' linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mchezo huo duniani, litapigwa jijini hapa Oktoba 5.
Huo
utakuwa utetezi wa kwanza kwa Klitschko, dhidi ya nkali huyo wa
masumbwi raia wa Russia, ingawa mazungumzo ya mkataba wa mtanange huo
hayajafikia tamati.
"Tunaweza
kukutana mapema iwezekanavyo," alisema Klitschko na kuongeza; "Hajawahi
kupoteza pambano lolote na katika hilo hakuna tatizo kwangu, kwani
namfahamu vema."
Kwa
upande wake Povetkin alisema: "Nina furaha kama pambano hilo
litakuwepo. Mimi naangalia mbele katika kukuktana na bondia huyo imara
ulingoni."
Wakati Klitschko, 37, ana rekodi ya kupanda ulingoni katika mapambano 63 na kushinda mara 60, yakiwamo 52 ya KO, Povetkin ana rekodi ya kushinda mapambano yake yote 26, yakiwamo 18 ya KO.
0 comments:
Chapisha Maoni