Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distileries
Limited (TDL), David Mgwassa, akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari, Dar es Salaam, kuhusu kuiomba serikali kuondoa kodi inayotoza
kiwanda hicho kutokana na ununuzi wa zao la zabibu kwa kuwa bado
hakijajiimarisha kiuzalishaji. Kushoto ni Mwakilishi wa waandishi wa
habari wa kiwanda hicho, Spear Patrick.
Mgwassa akijibu maswali kutoka kwa wanahabari
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
UONGOZI wa Kiwanda cha Konyagi
cha Tanzania Distileries Limited (TDL), umeiomba serikali kuondoa kodi
inayotoza kiwanda hicho kutokana na ununuzi wa zao la zabibu kwa kuwa
bado hakijajiimarisha kiuzarishaji.
Ombi
hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwassa katika
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam ambapo
alielezea wasiwasi wa zao kuja kudorora iwapo kodi hiyo itaendelea
kutozwa.
Alisema
kutokana na uendeshaji wa kampuni kwa miaka sita tangu ifufue mashamba
ya zabibu miaka saba iliyopita kwa kuagiza mbegu kutoka Afrika Kusini ni
kipindi kifupi kuanza kukatwa kodi. “Kipindi
cha miaka sita kuanza kukatwa kodi ni mapema mno kwani bado
hatujasimama sawasawa tunaomba serikali kuangalia kwa makini jambo hilo
ili kunusuru kilimo cha zao hilo na kuwakomboa wakulima” alisema
Mgwassa.
Alisema
TDL kwa mwaka huu imenunua lita milioni 1.720 za zabibu na kuwa lita
milioni 1.1 ni kwa ajili ya kinywaji cha Valuer na 0.7 zilienda kwenye
bidhaa nyingine. Mgwassa
alisema kwa mwaka jana kampuni hiyo imetumia sh.bilioni 1.8 kwa ajili
ya kununua zao hilo ambapo mwaka huu watatumia bilioni 2.3 na kuwa hali
ya kilimo cha zao hilo ni nzuri pamoja na soko lake tofauti ni
inavyodaiwa na baadhi ya watu.
Aliongeza
kuwa iwapo serikali itaendelea kotoza kodi hiyo upo uwezekano wa
vinywaji vinavyozarishwa na kiwanda hicho bei yake kuwa juu kutokana na
bei ya soko kulingana na ile ya vinywaji kutoka nje ya nchi.
0 comments:
Chapisha Maoni