1. Hivi
karibuni tumepata uhakika kuwa Tanzania Premier League (TPL) na Azam Media
wanayo nia ya kuingia mkataba wa kuonyesha mechi za Ligi Kuu (Premier League)
kwa msimu wa 2013/2014, 2014/2015 na 2015/2016
2. Baada ya
Kamati ya Utendaji ya YANGA kufanya uchambuzi wa kina juu ya taarifa ya
makubaliano ya kibiashara ya TPL / Azam Media ilihitimisha kuwamkataba huu
hauna maslahi kwa YANGA, na kwa hivyo, Kamati ya Utendaji ya YANGA ilifikia
uamuzi kuwa mechi za YANGAzisirushwe hewani na Azam Media.
Kwa kuwa wawazi, Kamati ya Utendaji ya
YANGA ilitoa taarifa kwa wanachama wa YANGA kupitia vyombo vya habari tarehe 29
Julai, 2013 ambapo iliweka bayana sababu zake na kueleza kuwa YANGAhaina tatizo
na vilabu vingine vya mpira wa miguu ikiruhusu mechi zao kurushwa na Azam
Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mechi zake za
Vodacom Premier League katika Azam Television.
3. Sote
tumeona baada ya hapo kuwa “nguvu ya ziada” inatumika kupotosha msimamo wa
Kamati ya Utendaji ya YANGA na kuidhalilisha Klabu ya YANGA hadharani
Juu
ya hayo Na Kwa kushangaza Sana, baadhi ya vilabu vya mpira WA miguu ambavyo
vina sifa kuwa havijawahi kushinda Ligi Kuu, vimeundwa hivi juzi tu, havina
uzoefu wowote WA kucheza soka kimataifa n.k. vina kuja kuyapanga Kamati ya
Utendaji ya YANGA jinsi ya kuendesha shughuli za Klabu ya Yanga, vikiwa
vinasahau vilabu vyao wenyewe na badala yake kuiingilia YANGA kwa sababu
zinazojionyesha wazi.
Inadhihirika
wazi kwamba kuna ushirikiano usio mzuri unaoashiria kula njama kuilazimisha
YANGA iruhusu mechi zake zirushwe na Azam Television.
Kwa
kuwa YANGA ni Klabu ya Wanachama yenye kupata nguvu kutokana na misingi yake ya
kidemokrasia iliyojijengea na uamuzi wake wa mwisho unatokana na Wanachama wake
mwenyewe, umeamua kuliweka suala hili zima kwa Wanachama wa Yanga ili waamue ni
njia gani ya kufuata kwa maslahi ya Klabu yetu.
Kwa
kuzingatia hali hiyo basi, na kulingana na mamlaka niliyonayo kama Mwenyekiti
wa YANGA, natangaza mkutano wa dharura wa Wanachama wa YANGA tarehe 18 Agosti,
2013 utakaofanyika uwanja wa Sabasaba kwenye ukumbi wa PTA saa 3.30 asubuhi
waje tujadiliane na kuamua suala la Azam Television kurusha mechi za YANGA.
0 comments:
Chapisha Maoni